• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Madiwani na Wataalamu kutoka Nchini Kenya Wafanya ziara ya Mafunzo Jijini DSM

Posted on: August 26th, 2024

Halmashauri ya jiji la  Dar es Salaam leo tarehe 26 Agosti, 2024  wamepokea Ujumbe wa viongozi na wataalam kutoka Jimbo la Kilifi  Nchini Kenya waliofika kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika eneo la ukusanyaji wa mapato pamoja na utekelezaji wa miradi.

Wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Arnatoglou Jijini humo, Wataalumu hao waliweza kujifunza namna mbalilimbali Jiji la Dar es Salaam linavyofanya kazi zake katika eneo la ukusanyaji wa mapato pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali za kuongeza mapato pamoja na kusimamia miradi kwani kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mapato yameongezeka kwa kasi kutokana na kuanzishwa kwa kanda za huduma ambazo zimekua chachu ya ongezeko la asimia 105% ya mapato ya ndani ya Halmashauri ukilinganisha na mwaka 2022/2023 .

Sambamba na hilo, Waheshimiwa hao Waliweza kujifunza mbinu mbalimbali za uwekezaji ambapo kwa Jiji la Dar es Salaam wamewekeza kwenye masoko kwani kuna mpango wa ujenzi wa masoko ya kisasa matatu ambayo yatakua Chachu ya kuongeza mapato kwa Jiji kwani muundo wa ujenzi wa masoko hayo ni rafiki na utakua na eneo la maegesho la kulipia hivyo kupitia maegesho hayo Halmashauri pia itapata mapato zaidi.

Akiongea wakati wa Mafunzo, hayo Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndg. Elihuruma Mabelya ameeleza kuwa “Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amekua mstari wa mbele kuhimiza ushirikiano na mahusiano mazuri na nchi za jirani,  hivyo nitumie nafasi hii kuwakaribisha sana katika jiji letu, Tubadilishane mawazo na mbinu mbalimbali kwa  maslahi ya wananchi wetu tunaowaongoza . Mafanikio haya tunayoyapata yanatokana na juhudi, bidii pamoja na mshikamano  kati ya madiwani wetu na wataalamu. hivyo niwaombe Madiwani  kutoka Kilifi  mkatekeleze vyote mlivyojifunza bila kusahau ushirikiano na watalamu kwani wao ndio watendaji wakuu”.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati wa Fedha na Mipango ambaye ni mwakilishi wa Wadi ya Kaloleni Jimbo la Kilifi Mhe. Birya Fondo  amempongeza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam pamoja na watendaji wote kwa kuweza kushirikiana vyema katika kukuza mapato ya Jiji pamoja na usimamizi na utekelezaji  mzuri wa miradi huku akiahidi kwenda kufanyia kazi yote waliyojifunza.

“Kipekee naomba kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa mapokezi mazuri kutoka kwenu na pia kujitoa kwenu kutupatia Elimu hii ya ukusanyaji wa  kodi na utekelezaji wa Miradi , Hakika ziara yetu imekua yenye mafanikio makubwa kwani tumejifunza mambo mengi na mazuri na tutayafanyia kazi pindi tutakaporejea Kilifi“  Amesema Mhe. Birya

Aidha, Madiwani na watalamu hao Waliweza kutembelea Soko la Kimataifa la Samaki Feri pamoja na Soko la Kisutu kujifunza namna Jiji la Dar es Salaam linavyoendesha masoko hayo katika kuhakikisha mapato yanaongezeka.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.