Waheshimiwa Madiwani pamoja na Watumishi kutoka Halmashauri yaJiji la Mwanza, leo tarehe 7 Novemba, 2022 wamefanya ziara ya mafunzo Jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuimarisha utendaji kazi pamoja na kudumishamahusiano kati ya Halmashauri hizo mbili.
Wakiwa kwenye ziara hiyo, Waheshimiwa Madiwani na Watumishi waHalmashauri ya Jiji la Mwanza walipata fursa ya kujifunza mambo mbalimbaliikiwemo njia zinazotumiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katikaukusanyaji wa mapato, usimamizi wa miradi ya Maendeleo pamoja na eneo la Utawala Bora.
Aidha, ziara hiyo ilianza kwa kikao kilichofanyika katikaUkumbi wa mikutano wa Arnatoglou ambapo msafara kutoka Jiji la Mwanzaulipokelewa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Omary Kumbilamotona Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo, Ndugu Mafuru, ambapo walipata nafasi yakujadiliana mambo mbalimbali sambamba na Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Utawalapamoja na timu ya Menejimenti Jiji la Dar es Salaam.
Wakati wa uwasilishaji wa mada mbalimbali kutoka kwa Wataalm waJiji la Dar es Salaam waliwaeleza timu kutoka Jiji la Mwanza mbinu elekezikatika kuibua vyanzo mbalimbali vya mapato na kuwa kinara mara kwa mara katikaukusanyaji wa Mapato nchini na kuweza kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleokwa kutumia Mapato yake ya ndani, ikiwemo ujenzi wa masoko, shule, vituo vyaafya, barabara na hata kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na wageni hao ni Soko laKisasa la Kisutu na Machinjio ya Kisasa ya Vingunguti,ambayo imetekelezwa kwakutumia Mapato ya ndani ya Halmashauri."Halmashauri ya Jiji la Dar esSalaam ina miradi mikubwa kulingana na uwekezaji unaotokana na Mapato kuwamazuri,pia uwepo wa miradi ya kimkakati Kama soko Kuu la Kisutu na machinjio yaKisasa ya Vingunguti imeibuliwa kutoka hatua za chini Kama ilivyo Halmashaurizingine" amesema Mchumi wa Jiji la Dar es Salaam Bw.Hando.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.