Waheshimiwa Madiwani na wajumbe wa Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji Isaya Mwita Charles leo tarehe 18 Septemba, 2018 wamekutana katika ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya Mkutano wa Baraza wa robo ya nne ya mwaka kwa kipindi cha Aprili hadi Juni, 2018.
Mkutano huo wa Baraza pia umehudhuriwa na wananchi mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam ambao wamepata fursa ya kusikiliza mawasilisho ya taarifa za kila siku na za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutoka kwa Wenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uongozi, Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu, Kamati ya Huduma za Jamii, Kamati ya Mipango na Uratibu pamoja na Kamati ya Maadili.
Katika Mkutano huo Wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji pia walipata fursa ya kuuliza maswali ya papo kwa papo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kupata maelezo ya ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa ujenzi wa Kituo kipya cha Mabasi cha Mbezi Luis, kuboresha miundombinu ya Dampo, ujenzi wa vyoo vya Umma na utoaji wa huduma unaoepusha usumbufu kwa jamii.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.