Wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji, Isaya Mwita leo tarehe 23 Februari, 2018 wamefanya Mkutano wa Baraza katika ukumbi wa Karimjee na kujadili utekelezaji wa mpango na bajeti ya Halmashauri ya mwaka 2017/2018 kwa kipindi kinachoishia Desemba, 2017.
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika bajeti ya mwaka 2017/2018 iliidhinisha jumla ya Shilingi 22,025,888,000.00 ikiwa ni bajeti ya Mishahara ya watumishi, matumizi ya kawaida na za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Wananchi na wadau mbalimbali wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamepata fursa ya kushiriki Mkutano huo na kusikiliza mawasilisho ya taarifa za utekelezaji za shughuli za kila siku na za miradi ya maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.