Mashindano ya Mstahiki Meya wa Jiji wa Dar es Salaam Isaya Mwita ya Ndondo CUP yamemalizika ambapo timu ya Sober FC imeibuka mshindi na kujinyakulia kombe, jezi pamoja na mbuzi dhidi ya mahasimu wao Soweto FC.
Katika mashidano hayo ambayo yalikuwa na mvuto wa aina yake, yalihudhuriwa na wananchi mbalimbali, viongozi akiwemo mbunge wa jimbo la Temeke Mhe. Abdallah Mtolea na Waheshimiwa Madiwani.
Awali mashindano hayo ambayo yalikuwa na ushidani mkali yalihusisha timu 20 ambapo hadi kufikia fainali hapo timu mbili za Sober FC na Soweto ndio ziliweza kushiriki hatua hiyo.
Katika mchezo huo ambao ulifanyika katika viwanja vya Mzimuni Kata ya Vijibweni ambapo Meya Mwita ni Diwani wa kata hiyo, timu ya Sober ilipata ushindi kupitia kwa mchezaji wao Hassan Gumbo ambae aliipatia timu yake goli la ushindi dakika za lala salama.
Aidha katika mashindano hayo, mshindi wa pili ambaye ni Soweto walijinyakulia zawadi ya jezi pea moja pamoja na mpira huku mshindi wa tatu ambao ni Nondo FC iliibuka na zawadi ya mbuzi. Akikabidhi zawadi hizo kwa washindi Meya Mwita ambaye ndio mwaandaji wa mashindano hayo, na Diwani alisema lengo ni kuwaweka vijana pamoja kwa kuwa michezo ni furaha.
Alifafanua kuwa mashindano ya mwaka huu yalihusisha timu kutoka Kata moja ya Vijibweni na mashindao yajayo yatahusisha timu kutoka Kata mbalimbali ambazo zitapenda kushiriki.
Katika mashindano hayo zawadi nyingine zilizotolewa ni pesa tathilimu Shilingi 50,000 ambayo ilitolewa kwa mchezaji bora Ibrahimu Kadabla kutoka timu ya Nondo FC.
Hata hivyo Mbunge wa Temeke Mhe. Mtolea alisema kuwa katika mashindano yajayo timu 13 kutoka jimboni kwake zitashiriki.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.