Na: Shalua Mpanda
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema mikopo inayotolewa na halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kupitia makusanyo yake ya ndani(mikopo ya asilimia 10),imeweza kukuza mitaji na kuboresha biashara kwa wajasiriamali.
Mpogolo ameyasema hayo wakati wa kutembelea na kukagua mabanda ya wafanyabiashara wajasiriamali waliowezeshswa kupitia mikopo hiyo katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara 'Sabasaba" ndani ya viwanja vya Maonesho hayo vilivyopo wilayani Temeke.
Aidha amewataka wajasiriamali hao kutumia mikopo hiyo kama njia ya kujikwamua kiuchumi huku akisisitiza matumizi sahihi ya mikopo hiyo.
"Nimshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mikopo hii ambayo imekuwa chachu ya mabadiliko chanya ya kiuchumi kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu". Alisema
Mkuu huyo wa Wilaya amewahakikishia wajasariamali hao kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha inaendelea kutoa mikopo hiyo isiyo na riba kwa vikundi ambavyo vitakidhi vigezo na kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025, Halmashauri ya Jiji imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 18 ambazo zimeshaanza kutolewa kwenye vikundi.
Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam inashiriki Maonesbo haya ya 49 ya Biashara ya Kimataifa na imesogeza huduma mbalimbali zikiwemo utoaji wa leseni mbalimbali, elimu na ushauri wa kitaalamu pamoja na huduma nyingine.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.