• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Zaidi ya Trilioni 1 kutekeleza Miradi ya Barabara Mkoa wa DSM

Posted on: October 24th, 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb) ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kuhakikisha inaendelea kuboresha huduma kwa Watanzania kupitia Mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar esSalaam (DMDP) kwa awamu ya pili ukiwa na zaidi ya Shilingi Trilioni 1.18 sawa na Dola za Kimarekani Milioni 447.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba nane ya ujenzi wa miundombinu ya barabara katika Halmashauri tano za Mkoa wa Dar es Salaam kupitia DMDP awamu ya pili leo Octoba 24, 2024 iliyofanyika katika viwanja vya MwembeYanga Temeke Dar es Salaam, Waziri Mchengerwa ameeleza kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha miundombinu inaboreshwa ili wananchi wapate huduma bora na kwa wakati.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema mradi huo unajumla ya kilometa mraba za lami 250, mifereji yenye kilometa 90, stendi za mabasi tisa pamoja na masoko 18 ambapo kwa hatua ya awali mikataba inayosainiwa inaenda kutekeleza miradi ya barabara zenye urefu wa Km 63.66 zikiwa na thamani ya shilingi bilioni 190 katika Halmashauri tano za Mkoa wa Dar es Salaam huku zabuni 11 zilizobaki zenye jumla ya Km 104.56 zinatarajiwa kukamilika na Mikataba kusainiwa ndani ya Mwezi Novemba.

"Jambo hili linaonesha nia nje ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam, ambapo unatarajiwa kuboresha miundombinu mbalimbali barabara, masoko, vituo vya mabasi pamoja na miradi ya taka ngumu hivyo niwaagize Katibu Mkuu TAMISEMI na Mtendaji Mkuu wa TARURA kuhakikisha mnasimamia vizuri utekelezaji wa miradi hiyo ikamilike kwa wakati na ubora, kwani muda hautaongezwa kwa mkandarasi yoyote asipokamilisha kwa wakati." Amesisitiza Mhe. Mchengerwa.

Sambamba na hilo, Mhe. Mchengerwa amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha anawasimamia wakandarasi hao ili waweze kukamisha miradi hiyo kwa wakati huku akiwasisitiza kuhakikisha wanazingatia uhitaji wa wananchi, katika utekelezaji wa mradi hiyo, isijengwe maeneo ambayo sio rafiki na wananchi, hivyo wahakikishe masoko zaidi ya 20 yatakayojengwa yanajengwa penye uhitaji huku akizitaka Halmashauri zote kuhakikisha wanawajengea uwezo wafanya biashara.

Awali akiongea wakati wa hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kundelea kuboresha huduma za wananchi kwani miradi hii itaenda kuboresha miundombinu pamoja na kurahisisha usafiri kwa  watanzania huku akimuhakikishia kutekeleza yale yote atakayo ya agiza sambamba na kuhakikisha anawasimamia wakandarasi wote ili waweze kukamilisha kazi kwa wakati.

Aidha, kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mradi wa DMDP awamu ya pili kwa mikataba ya awali itaenda kutekeleza mradi wa mkataba mmoja wa  barabara za Km 9.2 zenye thamani ya shilingi bilioni 30.3 chini ya Mkandarasi M/s Jiangxi Geo- Engneering Group Corporation Ltd. ambapo barabara hizo ni pamoja na barabara ya  Kitunda - Kivule - Msongola yenye urefu wa Km 6.25 na barabara ya Kivule - Majohe Junction yenye urefu wa Km 2.77.





Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.