Na Mariam Muhando.
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndg. Elihuruma Mabelya ameendelea na utaratibu wake wa kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo kila siku ya jumamosi ambapo Tarehe 22.02.2025 ametembelea miradi mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Wilaya ya Ilala ya Kivule, Kituo Cha Afya Mvuti na Stendi ya daladala Chanika ambayo inatarajia kukamilika hivi karibuni.
Mkurugenzi Mabelya ameambatana na Viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Vitengo,Watalaamu kutoka Jiji, Wenyeviti wa Kamati za bodi za Ujenzi wa maeneo husika, Watendaji Kata, Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa na Madiwani wa kata husika.
"Kupitia Fedha za Mapato ya ndani tunatenga zaidi ya asilimia 70 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo hivyo ninamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kutuletea fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo itakayokwenda kuwasaidia Wananchi kupata huduma karibu karibu zaidi na kuwainua kiuchumi. " Alisema Ndg. Elihuruma Mabelya.
Mkurugenzi Mabelya amesema stendi ya Chanika ikikamilika itakwenda kurahisisha shughuli za Usafirishaji, ukusanyaji wa Mapato pia anatarajia itakwenda kuhudumia hata Mabasi yaendayo Mikoa ya jirani ambapo amewahakikishia Wananchi kuwa wajiandae kuitumia kwani itakwenda kuleta matokeo chanya.
Pia, Mkurugenzi wa Jiji hilo amewataka Wakandarasi kufuata sheria, kanuni na matakwa ya mikataba yao ili wakamilishe miradi kwa wakati maana kukamilika kwake kutaendelea kutatua changamoto za Wakazi wa Jiji la Dar es salaam.
Aidha, Mkurugenzi Mabelya ameendelea kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha za maendeleo anazozileta Halmashauri ya Jiji kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.