Na: Shalua Mpanda
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Elihuruma Mabelya amekutana na kufanya kikao cha siku mbili na wakuu wa Idara, Kanda na mameneja wa vyanzo vya mapato ili kuweka mikakati ya ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2025/2026.
Akizungumza katika siku ya pili ya kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Protea Courtyard Jijini humu, Mabelya amesema kwa mwaka wa fedha uliopita wameweza kuvuka lengo kukusanya Shilingi bilioni 132 sawa na asilimia 102.
Aidha, amewataka watendaji hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii kumsaidia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ana lengo la kuwaletea wananchi maendeleo kupitia makusanyo hayo.
"Niwapongeze kwa kazi nzuri mliyoifanya, ila pongezi hizi ziambatane na utendaji kazi ili kuweza kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato tuliyojiwekea kwa mwaka huu". Alisema
Kikao cha leo ni muendelezo wa kikao kazi kilichofunguliwa rasmi jana chenye lengo la kutathmini mwaka wa fedha uliopita pamoja na mafanikio ya kibajeti na kuangalia mustakabali wa mwaka mpya wa fedha 2025/26.
Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwa mwaka huu wa fedha 2025/2026 imepanga kukusanya makusanyo ya zaidi ya shilingi bilioni 152.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.