Wafadhili kutoka Ismail Civic leo tarehe 2 Septemba, 2023 wamemkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam matundu 51 ya vyoo katika Shule ya Msingi Umoja wa Mataifa pamoja na Shule ya Msingi Muhimbili ikiwa ni sehemu ya mchango wa wadau wa elimu kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira bora na tulivu.
Akiongea katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndg. Jomaary Satura amewashukuru wadau hao kwa kutoa kipaumbele katikasekta ya elimu nchini huku akiwaahidi kuendelea kushirikiana nao katika kujenga na kuimarisha sekta ya elimu nchini.
“Nipende kuipongeza taasisi ya Ismail Civic kwa kuiunga Mkono Serikali kutatua matatizo mbalimbali katika Sekta ya Elimu. Naahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwenu , pia nitoe wito kwa wanafunzi mvitumie vyoo hivyo kwa matumizi sahihi na siyo kuharibu miundombinu yake." Ameeleza Ndg. Satura.
Zoezi hilo pia liliambatana na utoaji wa vyeti vya shukrani kwa wadau wa waliotoa mchango kufanikisha ukarabati wa vyoo hivyo ambao ni Aga Khan Council of Tanzania, Diamond Trust Bank, National Bank of Commerce, Honest Logistics LTD, Mansoor Industries Limited (MOIL), Jubilee Allianz Insurance, Nas Tyre Service LTD, Bhanji Transport, Mehta Integra International, River Oil, Tanga Mining Company LTD pamoja na Furnicom Tanzania LTD.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.