Na. Judith Msuya
Kuelekea Sensa ya watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Maendeleo endelevu ya Tanzania Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Amos Makalla leo Februari 15, 2022 amefanya kikao kazi na viongozi mbalimbali wa Halmashauri tano(5) za Mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Halmashauri ya Maniapaa ya Kinondoni , Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni lengo likiwa kuelimisha, kuhamasisha na kujua mpango kazi wa kwaajili ya anuani za Makazi ambazo ni msingi mzuri wa Sensa ya Makazi ya Mwaka 2022.
Kikao kazi hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Arnatoglou Jijini Dar es Salaam kilichowajumuisha viongozi mbalimbali wakiwemo Kamisaa wa Sensa ,Mwakilishi kutoka Wizara ya Habari na Mawasiliano, Wakuu wa Wilaya zote tano, Mameya wa Halmashauri zote tano, Wakurugenzi wa Halmashauri zote, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, wataalamu wa takwimu Pamoja na maafisa Ardhi kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla amewaelekeza wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam kuharakisha mpango kazi wa oparesheni ya zoezi la anuani za makazi ambslo ndio msingi mzuri wa kufanikisha zoezi la sensea ya Wat una Makazi ya Mwaka 2022 inayotarajiwa kuanza mwezi wa nane mwaka huu.
Sambamba na hilo RC Makalla amesema zoezi hilo lina manufaa makubwa kwakua linakwenda kuweka Jiji katika mpangilio mzuri kwani migogoro ya ardhi itapungua suala la ulinzi na usalama litaimarika, majanga ya moto yatapungua na litawezesha biashara kidijitali hivyo ametoa wito kwa wananchi kulipokea vizuri na kutoa ushirikiano ili kukamilisha zoezi hili kwa wakati.
Hata hivyo Mhe. Makalla amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta zoezi hilokwa wakati muafaka ambao una mapinduzi makubwa ya sayansi na Teknolojia na mambo mengi yanakwenda kwa mfumo wa kidijitali.
Vilevile Mhe. Makalla amewapongeza Viongozi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki katika zoezi zima la kuwapanga wafanyabiashara Pamoja na maandalizi mazuri waliyoyafanya kupendezesha na kusafisha Mkoa wa Dar es Salaam kwani Mkoa wa Dar es Salaam umekua ni miongoni mwa Majiji safi barani Afrika ambapo Mkoa wa Dar es Salaam umeshika nafasi ya sita(6) hii inaonyesha ni jinsi gani zoezi la kupendezesha na kusafisha Dar es Salaam limeweza kufanyika vizuri na kwa utaratibu mzuri.
Kwa upande wake Kamisaa wa Sensa Mhe. Anna Makinda ameeleza kua "japo zoezi hili anuani za makazi ni gumu kutokana na asili ya Mkoa wetu wa Dar es Salaam lakini nawaomba mlifanye kwa umakini mkubwa na weledi kwa kushirikiana na wataalamu wetu Wa takwimu kusudi shilingi Bilioni 28 zilizotengwa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan zitumike kwa uhakika na kazi iwe nzuri na tuimalize kwa wakati japo muda ni mchache.”
Akitoa taarifa fupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam juu ya utekelezaji wa mpango kazi wa ukusanyaji taarifa za Anuani za Makazi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu ameeleza kua Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imejipanga vizuri katika kuratibu zoezi la ukusanyaji wa taarifa kwani imeweza kuwajengea uwezo Watendaji wa mitaa na Kata ili waweze kusimamia vizuri ukusanyaji wa takwimu hizo.
“Tarehe 14, Februari 2022 Halmashauri ya Jiji ilifanya Kikao na Watendaji Kata na MItaa Pamoja na Waratibu lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo juu kusimamia zoezi zima la Anuani za Makazi Pamoja na kuwapa maelekezojuu ya kufanya kazi zilizopo chini yao, pia Kutokana na kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ina Kata 36 na mitaa 159 ambazo zina Idadi ya kaya 486138 hivyo ilikufanikisha kazi hii tutahitaji wakusanya data mia tatu kumi na nane (318) na muda wa utekelezaji kulingana na mpango kazi ni siku sitini (60) hivyo tumepanga ratiba ya kuwajengea uwezo watu wote watakaohusika katika kazi hii ambapo tarehe Februari 17 tutawajengea uwezo watendaji Kata na Mitaa na februari 23, 2022 tutawajengee uwezo wakusanya taarifa namna ya kufanya kazi hiyo na mnamo Februari 23, 2022 zoezi la kukusanya taarifa za Anuani za Makazi litaanza rasmi na hadi kufikia April 23, 2022 zoezi hilo litakua limekamilika.”Ameeleza Bi. Tabu Shaibu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.