• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam atoa Maelekezo 17 kwa watendaji wa Sekta ya Ardhi na Mipangomiji

Posted on: May 18th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul C. Makonda leo 18 Mei, 2017 amezungumza na Watendaji wa Idara ya Ardhi na Mipangomiji wa Halmashauri za Dar es Salaam wakati wa kikao kazi cha kujadili changamato mbalimbali zinazoikumba sekta ya Ardhi ikiwa ni pamoja na migogoro isiyokwisha ya umiliki wa ardhi.

Katika kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Arnatouglou, Mhe. Makonda alitoa maagizo yafuatayo;

  1. Watendaji wa Sekta ya Ardhi na Ujenzi  Kushughulikia migogoro ya Ardhi na Ujenzi ili wananchi wasipeleke malalamiko yao ngazi za juu.
  2. Watendaji wa Sekta ya Ardhi na Ujenzi Wameagizwa kutoa vibali vya Ujenzi ndani ya mwezi mmoja na zoezi hilo lianze mwezi Juni mwaka huu wa 2017. Mwanzoni mwa mwezi Julai, 2017 kuzinduliwa teknolojia ambayo wananchi watapata taarifa zao za Ardhi kwenye mtandao jambo ambalo litafanya Dar es Salaam kuwa kiganjani mwa wananchi.
  3. Wakuu wa Idara katika Sekta ya Ardhi na Ujenzi  kuhakikisha wanatoa taarifa kuhusu Mipango ya Idara kwenye vyombo vya habari kwa kuwatumia maafisa habari kwani tayari wana mahusiano na waandishi mbalimbali katika vyombo vya habari.
  4. Wakuu wa Idara ya Ardhi na Ujenzi kutoa TAARIFA ya maeneo yote ya wazi yaliyotolewa Hati, na kujitokeza haraka kwa wote waliotoa Hati za maeneo ya wazi kama wapo.
  5. Wakuu wa Idara ya Ardhi Na Ujenzi kusimamia haraka upimaji wa maeneo yote ya Umma kama kama vile Shule, Hospitali, na Masoko kama alivyoagiza Waziri wa TAMISEMI sambamba na kutoa Mikakati ya Upimaji.
  6. Wakuu wa Idara ya Ardhi na Ujenzi kuhakikisha ufanisi na bidii ya utendaji inaongezeka hususani mikakati ya kuhusisha wapimaji binafsi wanaotambulika kwani Mji ukipimwa vyema Madiwani watafurahi lakini pia itakuwa njia rahisi ya kuepuka migogoro ya Ardhi.
  7. Kushughulikia changamoto za kisera zinazofanya utaratibu wa Upimaji na utoaji wa Hati kuchelewa kukamilka.
  8. Mabaraza ya Kata kuangaliwa upya kwa mujibu wa Sheria ili kuwa na utendaji imara unaoshabihiana na jambo la kisera.
  9. Kila Mtumishi kufanya kazi yake kwa uaminifu kwani dhamana aliyopewa ni kubwa na anapaswa kuitendea Haki. Watumishi wote kusimamia na kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani chama hicho ndicho kimeingia mkataba na wananchi katika kipindi cha miaka mitano.
  10. Kila Mkuu wa Idara kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015 - 2020 ili kutambua maelekezo yaliyobainishwa katika Sekta yake sambamba na kuwaelekeza wasaidizi wao pia kuisoma na kuielewa vyema Ilani hiyo.
  11. Kufatilia na kufahamu upandaji wa madaraja na stahiki zao kwani ni Haki zao za msingi kisheria ikiwa ni pamoja na kwenda likizo.
  12. Watumishi wote kuheshimu mamlaka walizonazo na kutumia vikao halali kutoa taarifa sahihi kwa watu husika.
  13. Kuwa na ushirikiano wa watumishi katika Idara zote ili kukuza ufanisi wa Kazi.
  14. Kujitokeza ndani ya wiki moja kwa watumishi wote wa Sekta ya Ardhi waliojihusisha na utoaji wa Hati za Ardhi kinyume na sheria na endapo wasipojitokeza na wakabainika watachukuliwa hatua za kisheria.
  15. Kufafanua baadhi ya mambo ili Madiwani waweze kuelewa sambamba na kutoogopa maazimio kama wanatenda kazi kwa mujibu wa Sheria pasipo kupendelea.
  16. Wakuu wa Idara kila mwisho wa wiki kutoa taarifa kwa Wakurugenzi inayoonyesha idadi ya Migogoro na jinsi ilivyotatuliwa.
  17. Katika kupunguza changamoto ya kuwafikia wananchi kwa Wakati Mkuu wa Mkoa amesema atatoa Pikipiki 5  kwa kila Manispaa za Jiji la Dar es Salaam, yaani jumla ya pikipiki 25 kwa Manispaa zote 5 za Sekta ya Ardhi kwa kila Manispaa.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.