Akizungumza na Wananchi wakati wa ukaguzi wa Kituo cha Afya Kinyerezi Mhe.Chalamila amesema “Kutokana na kasi ya ukusanyaji wa mapato pamoja na uratibu mzuri wa fedha kwa Jiji la Dar es Salaam Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kibali kwa Jiji la Dar es Salaam kutumi Bilioni 21 kwaajili ya ujenzi wa hospitali tatu katika kila Jimbo ambapo kila Hospitali itagharimu kiasi cha shilingi bilioni 7 na tayari bilioni 15 zimeshahamishwa na zitawekwa bilioni 5 kwakila kituo shikizi ambapo hospitali hizo zinaenda kujengwa hivyo tunaendelea kumshukuru Mhe. Rais kwa kuendelea kutekeleza Sera yake ya kuhakikisha huduma za kijamii zinawafikia Wananchi kwa wakati na kwa ukaribu zaidi”.
Sambamba na hilo, Mhe. Chalamila amewataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu kwani Serikali ya Tanzania ni sikivu na itaenda kutatua changamoto zilizosababishwa na mafuriko pamoja na changamoto za maji na umeme huku akieleza kuwa zaidi ya bilioni 50 zimetolewa kwaajili ya ukarabati wa Bonde la Mto Msimbazi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo ameendelea kumshukuru Mkuu wa Mkoa kwa ziara yake ya siku tatu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Ilala kwani ziara yake imekua ya mafanikio kwa wananchi na inaonyesha ni jinsi gani Serikali imekua mstari wa mbele kutatua shida za wananchi na kuboresha huduma za kijamii, pia amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kutekeleza maagizo yote aliyoyatoa kwa wakati.
Aidha Akihitimisha ziara yake ya Siku tatu katika Jimbo la Segerea Mhe. Chalamila amekagua Miradi mitatu ya maendeleo inayotekelezwa na kusimamiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ikiwemo mradi wa kiwanda cha Metro Steel - Kiwalani, ujenzi wa Ghorofa Shule ya Sekondari Minazi Mirefu pamoja na ukaguzi wa Kituo cha Afya Kinyerezi na kufanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.