Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amempongeza Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam pamoja na Madiwani katika ufuatiliaji,usimamizi na utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi katika eneo la uwezeshwaji wananchi kiuchumi.
Akihitimisha mafunzo yaliyoanza tarehe 28 Novemba 2022 na kumalizika tarehe 1 Disemba 2022 kwa majimbo yote matatu ya Ilala, Ukonga na Segerea huku siku ya kuhitimisha madiwani nao wameweza kupata mafunzo hayo.
Ludigija amesema hayo leo tarehe 1 Disemba 2022 katika kikao kazi cha madiwani pamoja na watendaji kata wa Halimshauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiwa wanapata mafunzo juu ya mfumo wa kusajili vikundi vya vijana,wanawake na watu wenye ulemavu ili kuweza kuomba mikopo hiyo katika ngazi ya Halmashauri.
"Nimshukuru Mstahiki Meya Omari Kumbi la moto pamoja na Baraza la Madiwani kwa usimamizi na ufuatiliaji mzuri wa utekelezaji wa ilani ya Chama cha CCM katika wilaya ya Ilala hasa katika eneo la uwezeshwaji wa wananchi kiichumi, Hongereni sana"
Kikao kazi hiko kimelenga kuwapa ufahamu madiwani,wetendaji kata pamoja na wakuu wa Idara kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ili kuweza kuendelea kusimami utekelezaji wa ilani ya chama kuweza kufikia malengo ya kuongeza kipato kiuchumi kwa wananchi wote ndani ya Halmashauri.
Aidha, Ludigija amesisitiza ushiriki wa Madiwani, Watendaji wa Kata pamoja na wakuu wa idara wote katika kupata elimu hii juu ya mfumo huu amabo utasimamia usajili wa vikundi ni hatua nzuri na bora kuweza kufikia malengo na namna pekee ya kuongrza ajira na kupunguza vijana kutegemea kuajiriwa katika sekta binafsi au serikali bali kupitia mikopo tunawapa fursa ya kujiajiri, amesema.
"Nimekuwa nikifuatilia mwenendo mzima wa uwezeshwaji wananchi kiuchumi kupitia asilimia kumi ya mapato ya ndani, nimeona kuna mambo mengi yanafanyika ambayo kimsingi bila ya ufuatiliaji wenu waheshimiwa pengine ufanisi ungekuwa na changamoto nyingi sana"
Katika kutekeleza Ilani ya Chama cha mapinduzi usimamizi ni muhimu na tutambue utoaji wa mikopo hii yote ni maelekezo kutoka kwa Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji huu wa ilani hivyo basi.
"Namshukuru na kumpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kwa kuona umuhimu wa kutoa mafunzo kwa watendaji mtaa,wenyeviti wa mtaa, Watendaji wa Kata, Wakuu wa Idara pamoja na madiwani kwa kuwapa mafunzo haya ya mfumo huu"
Vilevile, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam akitumia jukwaa hilo la mafunzo kwa madiwani amesema "Nashukuru sanaa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wetu Mpendwa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuanzisha mfumo huu ambao unakwenda kutatua changamoto nyingi katika eneo hili la mikopo,pia madiwani tukawe mabalozi katika kata zetu kusaidia wananchi".
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.