Na : Doina Mwambagi
Leo tarehe 18.02.2025 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo ametoa wito kwa wakandarasi kuzingatia masharti ya mikataba wanayoingia ili kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ufanisi na makubaliano waliojiwekea.
Akizungumza katika viwanja vya Karimjee wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba mitatu, Mhe. Mpogolo amesisitiza kuwa wakandarasi wanapaswa kuwa waaminifu katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia viwango vya kazi vilivyokubalika.
Sambamba na hilo, Mhe. Mpogolo pia amezitaka taasisi za kifedha kuwaunga mkono wakandarasi kwa kuwapatia mikopo itakayowawezesha kununua vifaa vya kisasa ili kuongeza ufanisi wa kazi zao.
“Ni muhimu kwa wakandarasi wetu kuwa na vifaa vya kisasa ili kuongeza tija na ubora wa miradi wanayotekeleza. Taasisi za kifedha zina nafasi kubwa ya kusaidia katika hili kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu,” amesisitiza Mhe. Mpogolo.
Mikataba hiyo, ambayo inalenga kuboresha sekta ya ujenzi na miundombinu katika Wilaya ya Ilala, inatarajiwa kuwa chachu ya maendeleo na ustawi wa wakazi wa eneo hilo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.