Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mheshimiwa Edward Mpogolo leo tarehe 15 Mei, 2024 amefanya kikao kazi na Watendaji wa Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam lengo likiwa ni kuwakumbusha watendaji hao kusimamia majukumu yao kwa kuhakikisha wanasimamia shughuli zote za kimaendeleo zinazotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Aidha, katika kikao kazi hicho Mhe. Mpogolo ametoa maelekezo kwa watendaji wote wa Mtaa kuhakikisha wanashirikiana na ofisi ya Mkurugenzi katika kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halamshauri ya Jiji la Dar es Salaam.
"Madhumuni ya kikao kazi hichi ni kufahamiana na kufahamu misimamo yetu katika kuhakikisha mnasimamia vyema miradi ya maendeleo inayotekezwa kwa kuhakikisha mnashirikiana baina yenu wenyewe pamoja na sisi viongozi wenu kwani mahusiano baina yetu ndio chachu ya maemdeleo katika Halmashauri yetu hivyo tuhakikishe tunasimamia suala la ulinzi na usalama katika mitaa yetu, usafi wa mazingira, miradi inayotekelezwa ndani ya mitaa yenu bila kusahau zoezi zima la ukusanyaji wa mapato lengo ni kuhakikisha Jiji letu linakua kwa kasi kila sekta”. Ameeleza Mhe. Mpogolo
Sambamba na hilo Mhe. Mpogolo ameendelea kusema "Haiwezekani Mkuu wa Wilaya nifanye majukumu yangu na pia nifanye majukumu yako Mtendaji wa Mtaa kwani majukumu yenu ni kumsaidia Mkurugenzi moja kwa moja kusimamia miradi, msiwaachie wanafunzi wa kujitolea ofisi kwani ni wajibu wenu kufika ofisini kwa wakati na kusimamia kazi zinazowahusu hivyo naomba mhakikishe mnasimamia na kutekeleza vyema majukumu yenu ya kazi na nitaanza ziara ya kutembelea mitaa yote kuona changamoto zinazowakabili na kuleta masuluhisho sahihi."
Kwa upande mwingine Mhe. Mpogolo amewasisitiza Watendaji wa Mtaa kuhakikisha wanashirikiana na viongozi kwa ukaribu zaidi katika maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Octoba, 2024.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Ndg. Jomaary Satura amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kikao kazi hicho cha kuwakumbusha majukumu yao na kumhakikishia kuwa wanaenda kutekeleza yale yote aliyoyaagiza ikiwemo ukusanyaji wa mapato pamoja na usimamizi wa miradi inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa maendeleo ya nchi huku akiwahakikishia watendaji wa mtaa kuboresha stahiki zao baada ya wao kufanya kazi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.