Na,amanzi kimonjo.
Kwa niaba ya Mkuu wa Dar es Salaam,Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James leo tarehe 16 Octoba 2022 ametembelea maonesho ya maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam,maadhimisho hayo yamefanyika ikiwa yameudhuliwa na Halmashauri zote tano zilizopo Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni Halmashauri ya Ubungo,Temeke,Kinondoni,Kigamboni na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam (Ilala) huku Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa mwenyeji wa maonesho hayo.
Akimuakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.James ametembelea mabanda yote ya Halmashauri zote Tano "Nawapongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwa maandalizi makubwa katika mabanda yao kwa vitu vilivyojaa ujuzi na teknolojia katika maadhimisho haya ya chakula Duniani,endeleeni kufanya hivyo kwa maslahi mapana ya wananchi" amesema Mhe.James.
kila mwaka ifikapo tarehe 16 Octoba ni maadhmisho ya siku ya chakula Duniani Kauli mbiu katika maadhimisho ya mwaka huu inasema " Uzalishaji bora,Lishe bora,Mazingira bora na Maisha Bora kwa wote Habaki Mtu nyuma" ikiwa ni sehemu moja wapo ya kuhamasisha na kuhimiza Ulaji bora wa vyakula kwa afya njema kwa wote inawezekana, maadhimisho haya ni ya 77 tangu kuanza kusherekea kuadhimishwa kwake.
Shughuli za uzalishaji wa chakula kwa njia za kisasa za kilimo bora sambamba na hilo Mkoa wa Dar es s Salaam ikiongozwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inajikita zaidi na kilimo cha aina mbalimbali ikiwa pamoja na kilimo cha mboga,uyoga,Mahindi,matunda,papai,pilipili hoho na mazao mengi ikiwa nyenzo muhimu zitumikazo za kisasa kama vile kilimo cha mjini,kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia matone kwa chupa na kutumia mipira.
"elimu tuliyoipata leo ikatunufaishe,ikaelimishe juu ya matumizi ya chakula ili kudumisha lishe bora na umuhimu kila mtu kila mtu atumie maonesho haya kuweza kunufaika pia kauli mbiu ya mwaka huu inatutaka kama taifa kuweka mkakati mahususi wa kula chakula bora kutoka katika makundi yote sita ya vyakula kikamirifu"
Sambamaba na hilo kudumisha chakula Duniani teknolojia mbalimbali utumika katika kuandaa chakula inayotumia umeme wa jua,mashine za kukuna nazi,mashine za kutengeneza juisi,mashine za kuchepa mahindi na viungo kama tangawizi,uji wa lishe na zinginezo Halmashauri ya Dar es salaam ina maeneo makubwa kwa shughuli za kilimo kama Mbondole na Kinyamwezi.
Aidha Mhe.James amesisitiza matumizi sahihi ya vyakula kwa kudumisha lishe kwa afya bora kwa mwanadamu pia ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kudumisha lishe kwa watanzania "Nashukuru serikali ya awamu ya sita iliyochini ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mipango madhubuti juu ya lishe bora kwa watanzania na kuongeza bajeti katika uzalishaji,utoaji wa ruzuku ili kuimarisha sekta ya kilimo ili kukuza uzalishaji wa chakula".
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.