Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mhe. Omary Kumbilamoto leo tarehe 02, Octoba 2023 amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa soko la Vingunguti, huku akiwa ameambatana na Kamati ya Siasa Kata ya Vingunguti lengo likiwa ni kufuatilia Maendeleo ya ujenzi huo.
Akizungumza katika ziara hiyo Mhe. Kumbilamoto amesema “Sisi kama Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam tulitenga shilingi milioni 54 kwaajili ya ujenzi wa Soko hili lakini tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuwezesha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa soko la Vingunguti hii inaonesha jinsi gani Mheshimiwa Rais anavyotambua mchango wa wajasiriamali hadi kuamua kuwajengea Soko hilo la kisasa ambapo katika soko hili huduma zote muhimu zitapatikana kwani katika soko hili kutakua na mamalishe pamoja na wachonga vinyago kwani kutokana na machinjio yetu ya Vingunguti kuwa ya kisasa tunategemea kupata watalii kutoka nje hii Ndio sababu pekee ya kuwaweka watu wa Vinyago katika Soko hili la machinjio ya Vingunguti.”
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Vingunguti Ndg. Agatha Limbumba ameshukuru juhudi za Mheshimiwa Rais kwa kutoa fedha za kuwezesha ujenzi huo ambao ni chachu ya maendeleo katika kukuza sekta ya biashara nchi.
Naye Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Vingunguti Bw. Mohammed Mwarabu ametoa shukrani zake kwa viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kuwajengea soko la kisasa na kuahidi kulitunza soko hilo pindi watakapokabidhiwa.
Soko hilo la Kisasa la Vingunguti linatarajiwa kukamilika Novemba 2023 na Litagharimu shilingi milioni 500 pindi litakapokamilika.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.