Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe. Jerry Silaa ameshiriki hafla ya utiaji saini wa mkataba wa pili wa ujenzi wa shule ya Sekondari Kipunguni iliyopo katika Jimbo hilo.
Hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo imefanyika leo Januari 15, 2025 katika viwanja vya Shule hiyo.
Pamoja na mambo mengine, Mbunge huyo ameahidi kufunga mtandao wa mawasiliano (Internet) katika Shule hiyo mara baada ujenzi utakapokamilika ili wanafunzi waweze kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika masomo yao.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.