Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Bw. Ismail Ali Ussi, leo amekagua mradi wa kikundi cha vijana cha Ulipo Tupo kilichopo Tabata, Jijini Dar es Salaam.
Kikundi hicho chenye wanachama watano kinajihusisha na utengenezaji wa samani kwa matumizi ya nyumbani na ofisini kupitia kiwanda kidogo kilichowezeshwa na mkopo usio na riba wa shilingi milioni 150 kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia asilimia 4 ya mapato ya ndani kwa vijana.
Akizungumza na wananchi na vijana wa kikundi hicho, Bw. Ussi alisema: “Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliziagiza Halmashauri zote kutenga bajeti kwa ajili ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kupitia mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani.”
Aidha ndugu, Ismail Ussi ametoa wito kwa vijana kutumia fursa hiyo kujikwamua kiuchumi, huku akiipongeza Benki ya CRDB kwa kusimamia vyema mikopo ya vijana.
Kikundi cha Ulipo Tupo kimefanikiwa kushinda zabuni ya kutengeneza madawati 7,000 kwa Halmashauri ya Temeke na kuajiri vijana 40. Pia hushiriki katika shughuli za kijamii kwa kusaidia watoto wenye uhitaji.
“Jitokezeni kushiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa Utulivu na Amani,”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.