Naibu Meya Jiji la DSM Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Ojambi Masaburi amewataka Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanatekeleza dhima ya Sera na Utawala bora kama ilivyo katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Hayo ameeleza leo Januari 27, 2023 wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mzinga.
Akiongea katika hafla hiyo Mhe. Masaburi amempongeza Diwani wa Kata ya Mzinga kwa juhudi alizozionesha hadi kujengwa kwa ofisi hiyo kwani awali wananchi walikua wanapata changamoto za kupata huduma, hivyo baada ya ujenzi wa Ofisi hiyo ya Kata wananchi wa Kata hii wanapata huduma kwa ukaribu na haraka zaidi.
“Nimpongeze Diwani wa Kata ya Mzinga, Mhe. Isaack Job kwa kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kwa ukaribu zaidi na kuamua kujengwa Ofisi ya Kata ya Mzinga ambapo ofisi hiyo imegharimu takribani shilingi Milioni 100 ikiwa na vyumba 9 pamoja na ukumbi wa mikutano ambao utasaidia katika shughuli zote za kata.”
Sambamba na hilo Mhe. Masaburi ametoa wito kwa Madiwani wengine wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wana ainisha miradi yote iliyotekelezwa na Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzaniaza Samia Suluhu Hassan lengo likiwa ni kuhakikisha miradi hiyo inafuatiliwa kwa ukaribu zaidi.
Akitoa Shukrani zake, mmoja wa wakazi wa Kata ya Mzinga Bi. Neema Mapunda ameeleza kuwa “Kwanza kabisa napenda kumshukuru Diwani wa Kata ya Mzinga na Viongozi wetu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ujumla kwa ujenzi wa Ofisi hii kwani uwepo wa ofisi hii umeturahisishia upatikanaji wa huduma kwani awali tulikua tuanatembea umbali mrefu kutoka mzinga kwenda Kitunda kupata huduma za kiofisi pia nipende kumshukuru Mheshimiwa Rais ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuhakikisha wananchi tunapata huduma zote za kijamii kwa wakati na kwa ukaribu zaidi."
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.