Na: Doina Mwambagi
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mussa Zungu, leo tarehe 22 Juni 2025, amtembelea eneo litakapojengwa shule ya mfano inayojengwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Ujenzi wa shule hiyo ni sehemu ya jitihada za kuunga mkono sera ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mheshimiwa Zungu amemshukuru Benki ya CRDB kwa kuchukua jukumu la kijamii na kushirikiana na serikali katika kuboresha elimu. Anasema kuwa hatua hiyo inaonesha jinsi taasisi binafsi zinavyoweza kuwa washirika wa kweli katika maendeleo ya Taifa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, amesema kuwa benki hiyo imedhamiria kuhakikisha shule hiyo inakuwa ya mfano kwa kuwa na miundombinu bora na ya kisasa, sambamba na matumizi ya vifaa vyenye ubora wa hali ya juu kutoka kwa wakandarasi watakaohusika.
“Kwa kuwa shule hii itabeba jina la CRDB, tunategemea ijengwe kwa viwango vya hali ya juu vinavyoendana na hadhi ya benki yetu. Hili ni jambo la heshima kwetu, na tutalisimamia kikamilifu,” amesisitiza Nsekela.
Benki ya CRDB inasisitiza kuwa mradi huu ni sehemu ya mkakati wake wa uwekezaji wa kijamii (CSR) unaolenga kusaidia maendeleo ya sekta muhimu kama elimu, afya, na mazingira.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.