Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo ametoa wito kwa wenyeviti na wajumbe wa Serikali za Mitaa waliochaguliwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 27 Novemba 2024 kwenda kutoa huduma bora kwa wananchi na si kuwauzia.
Ameyasema hayo leo tarehe 28 Novemba ,2024 katika zoezi la uapishaji wa wenyeviti na wajumbe wa Serikali za Mitaa 2024, limefanyika katika ukumbi wa mikutano Anartoglou Jijini Dar es salaam.
Mhe. Mpogolo amesema “Napenda kutumia nafasi hii kutoa wito kwenu , mmechaguliwa na wananchi hivyo nendeni mkawatumikie kwa kutoa huduma bora na sio kuwauzia huduma , wananchi wana imani na nyinyi na ndio maana wamewachagua hivyo mkatende haki kwani kiongozi anayetenda haki eneo lake linakuwa na amani na utulivu”
Sambamba na hilo, Mhe. Mpogolo amesema kuwa Halmashauri yetu ni miongoni mwa Halmashauri zenye mitaa mingi, hata hivyo uchaguzi ulitamatika kwa amani pasipo vurugu wala vinyongo, hivi nampongeza sana Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam ambaye pia ni msimamizi mkuu wa Uchaguzi na timu yake kwa ujumla kwa kutii wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwakusimamia zoezi zima la Uchaguzi kwa haki,utulivu na weledi.
Kwa upande wake Mstahiki Meya Mhe. Omary Kumbilamoto amewataka viongozi hao kwenda kusimamia miradi iliyopo katika mitaa yao kwa maendeleo ya mitaa yao na taifa kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Ndg . Elihuruma Mabelya amewasisitiza viongozi hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia falsafa ya 4R (Reconciliation, Reforms, Resilience na Rebuild) ya Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kkufanya kazi ya kuwahudumia wananchi kwa haki na uzalendo kwa maslahi ya Jiji na Nchi kwa ujumla.
Halikadhalika, Wenyeviti na Wajumbe wa Serikali za Mitaa wamekula kiapo cha uaminifu, utii , katika kutimiza majukumu yao na kuwatendea haki watu wote kwa mujibu wa sheria.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.