• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

RC Chalamila aipongeza Halmashauri ya Jiji la DSM kwa uboreshaji wa Mazingira katikati ya Mji

Posted on: May 29th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa uboreshaji wa mazingira katikati ya Mji lengo likiwa ni kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linakua safi sambamaba na madhari nzuri.

Mhe. Chalamila ametoa Pongezi hizo leo Mei 29, 2024 wakati akiendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Jiji la Dar es Salaam katika Jimbo la Ilala, ambapo aliweza kukagua maeneo manne ya Kata ya Kivukoni ikiwemo Ujenzi wa barabara ya Mindu,Mradi wa Perving mtaa wa Ohio na Karimjee pamoja na kukagua mradi wa uzibuaji mitaro eneo ya IT-Plaza.

Akiongea na wananchi na wafanyabiashara waliokuwepo maeneo hayo, Mhe. Chalamila ameeleza kuwa kutokana na mazingira ya Mjini kati kuwa katika hali  isiyo ridhisha, Jiji la Dar es Salaam limechukua hatua stahiki ya kuhakikisha mazingira ya Mji yanakua safi na mandhari ya Jiji inapendeza kwani Dar es Salaam ndio kitovu cha kupokea wageni na mikutano mingi ya Kimataifa inafanyikia katikati ya Miji hivyo uboreshaji wa mazingira hayo ni chachu ya kuvutia wageni katika Jiji la DSM.

“Nipende kuipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa Hatua waliyoichukua ya kuboresha Jiji letu kwa kuweka perving na Kupanda miti na maua katika maeneo ya katikati ya Mji jambo linalofanya mandhari ya Jiji kuwa safi na kupendeza hivyo niwasisitize wafanyabiashara wote pamoja taasisi zote kutambua kuwa wajibu wao ni kuhakikisha Mji unakua safi pia napenda kuwapongeza Viongozi wa Jiji kwa kuchukua hatua ya kuzibua mitaro katika maeneo yaliyokua yanajaa maji wakati wa mvua kwani jitihada hizo zimepelekea kugundua kuwa kuna watu wanatiririsha maji machafu katika mifumo ya maji taka jambo ambalo linasababisha uchafu wa mazingira na kupelekea uwepo wa magonjwa ya milipuko, Sambamba na hilo nitaandaa kikao kazi kuzungumza na Watendaji wa Kata juu ya upendezeshaji wa Mji pamoja na kuongea na wadau na wamiliki wa majengo yote yalioko pembezoni mwa bararabara kutoka Airport hadi kufika Ikulu tuone namna gani tutapendezesha Jiji letu kwa kupanda miti pembezoni mwa barabara”.

Sambamba na hilo, Mhe. Chalamila amewataka PSSF pamoja na Ubalozi wa Canada kuhakisha ndani ya wiki moja wahakikishe wanatenganisha mfumo wa maji taka kwenye mfumo wa maji safi huku akiwataka wafanyabiashara wanaofanya biashara pembezoni mwa barabara katikati ya Mji waondoke na watafutiwe mahali sahihi pakufanya biashara zao ambapo wafanyabiashara wanaotambulika na sio kufanya biashara katika maeneo ya pembezoni mwa barabara ambayo ni mahususi kwaajili ya watembea kwa miguu.

Vilevile, Mhe. Chalamila ameweza kukagua ujenzi wa barabara ya Lindi ambapo amewaagiza Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dar es Salaam( DAWASA) wahakikishe wanashughulikia tatizo la maji taka katika barabara ya Lindi ambayo yamekuwa kero kwa Wananchi wa Kata ya Ilala na wafanyabiashara wanaozunguka eneo hilo huku akiwataka Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) kuhakikisha ndani ya wiki moja Mkandarasi anayetekelezaujenzi wa barabara ya Lindi anaanza ujenzi.

Awali akizungumza wakati wa Ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amesema “Baada ya kuona changamoto yaJiji la Dar es Salaam baadhi ya maeneo yanajaa maji wakati wa mvua tulichukua hatua stahiki za kuzibua mitaro maeneo ya Kamata, CBE pamoja na Muhimbili  ambapo tulibaini baadhi ya  majengo makubwa mifumo yao ya maji taka imeunganishwa kwenye mifumo ya maji safi, pia maeneo yote ya katikati ya mji yaliyowekwa pavings tunayatangaza kama Smart area na haturuhusu biashara yoyote kufanyika, hivyo nipende kukushukuru Mkuu wa Mkoa kwa ziara hii ndani ya Jimbo la Ilala kwani sisi kama Wilaya ya Ilala tutahakikisha mazingira ndani ya Jiji letu yanakua safi na tutaendelea kutekeleza yale yote uliyotuagiza lengo likiwa ni kuunga Mkono Juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kupendezesha Miji na kuwapanga wafanya biashara katika maeneo yao”.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo Cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Theresia Dennis ameeleza kuwa Jiji la Dar es Salaam liko katika kampeni ya uboreshaji wa mandhari katika maeneo yake ambapo shilingi bilioni 1.1 zimetumika kuboresha mandhari ya Jiji  katika maeneo 9 ya katikati ya Mji kuwekewa pavings pamoja na upandaji wa miti huku utekelezaji wa mradi huo ukiwa umekamilika kwa asilimia 95.












Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • Mwenge wa Uhuru waweka jiwe la Msingi Kituo cha Afya Mzinga

    June 03, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wakagua mradi wa vijana "Ulipo Tupo" Tabata

    June 03, 2025
  • Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Magengeni - Chang'ombe umewekewa jiwe la msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa

    June 03, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wazindua mradi wa Nishati Safi Soko la Samaki Feri

    June 03, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.