• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

RC Chalamila asikiliza na kutatua kero za wananchi wa Jimbo la Ukonga

Posted on: May 28th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila leo tarehe 28 Mei, 2024 amefanya mkutano wa hadhara wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Jimbo la ukonga ambapo ameahidi kutatua changamoto zinazowakabili wananchi hao.

Akiongea na wananchi kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye Viwanja vya Pugu, RC Chalamila amepokea changamoto mbalimbali zikiwemo za Miundombinu, masoko na migogoro ya ardhi ambapo zipo alizotatua papo kwa papo na nyingine kuzipatia utatuzi kwa kuwataka watendaji kuhakikisha wanazishughulikia.

"Niwaombe wananchi wa Jimbo la Ukonga Ili kupunguza migogoro ya ardhi na changamoto nyingine nawaasa kuchagua viongozi bora bila kujali itikadi zao za vyama, watakaoweza kumsaidia Mheshimiwa Rais kutekeleza nia aliyonayo kwa wananchi. Pia sisi viongozi tulioteuliwa na kuchaguliwa tufanye wajibu wetu kuhakikisha mambo yote yanakwenda sawa.” Amesema Mhe. Chalamila

Awali akifungua mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo ameeleza kuwa “Nitoe shukrani zangu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutatua kero ya miundombinu ya barabara kwa kutupatia zaidi ya Bilioni 231 kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya mwendokasi kuhakikisha wananchi wanapata usafiri kwa urahisi. Pia nikushukuru Mkuu wa mkoa kwa kuona haja ya kuja kusikiliza kero za wananchi wa Jimbo la Ukonga na nikuhakikishie tutazingatia haki katika kutekeleza yote utakayotuagiza."

Katika ziara hiyo RC Chalamila aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala , wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wilaya,  Viongozi wa Chama wa Wilaya ya Ilala, Wataalamu kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na wengine kutoka Taasisi zinazowahudumia wananchi kwa ukaribu ikiwemo Wakala wa Barabara za Vijijini na Mji (TARURA) , Wataalamu kutoka Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) pamoja na wataalamu kutoka Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO).

Nae Mstahiki Meya wa Jiji la DSM Mhe. Omary Kumbilamoto ameshukuru kwa ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa na kupongeza juhudi anazozifanya kuhakikisha anatatua kero kwa haki bila upendeleo , na kumuhakikishia kushirikiana nae na kutekeleza yale Yote aliyowaagiza.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.