Na: Judith Damas na Amanzi Kimonjo.
Katika kuendeleza Kampeni ya Usafi "safisha,pendezesha Dar es Salaam" Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Amos Makalla leo tarehe 24 Septemba, 2022 ameshiriki zoezi la usafi katika kata ya Mnazi Mmoja ambapo usafi huo hufanywa kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi.
Zoezi hilo la usafi lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam liliwahusisha Mkuu Wilaya ya Ilala,Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam ,Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam,madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,madiwani wa Manispaa ya Morogoro, Jeshi la Zimamoto, Watendaji kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Asasi mbalimbali ikiwemo ‘Juza Waste Pickere Initiative’ pamoja na wananchi wakiongozwa na vijana wa usafi kutoka Kajenjere Trading Company Limited.
Akizungumza katika zoezi hilo Mheshimiwa Amos Makalla amewata Wananchi kushiriki usafi kama desturi yao na sio kusubiri mpaka mwisho wa mwezi ufike ili kuweka mazingira safi na kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linapendeza na kuwa safi, "Nawapongeza wananchi wa Dar es salaam kwa kujitokeza na kushirikiana kufanya usafi,usafi ni afya kupitia usafi huu tutajikinga na magonjwamengi ikiwemo ugonjwa wa kipindupindu."
Aidha Jiji la Dar es salaam limekua na mvuto sana kutokana na kampeni hii na kwa sasa Mkoa huu ni wa mfano kwa Mikoa mingine katika kuhamasika kufanya hivi kwani leo tuna wageni ambao ni madiwani kutoka Manispaa ya Morogoro ambao wameweza kushiriki nasi katika zoezi la usafi hii ni jinsi gani Mikoa mingine imeweza kuuunga mkono zoezi la usafi lengo likiwa ni kuiweka nchi yetu ya Tanzania katika hali ya usafi.
"Sambamba na hilo pia Mheshimiwa Makalla amezindua magari mawili yatakayotumika kukusanya taka maeneo mbalimbali ndani ya Jiji la Dar es salaam,magari hayo yaliyo chini ya kampuni ya usafi inayotambulika kwa jina la Kajenjere trading company hivyo uwepo wa magari hayo utaimarisha usafi katika Jiji letu na Mkoa mzima wa Dar es Salaam.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mheshimiwa Ngw'ilabuzu Ludigija amewata Wananchi kushiriki usafi kama desturi yao na sio kusubiri mpaka mwisho wa mwezi ufike ili kuweka mazingira safi na kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linapendeza na kuwa safi, "Tuhakikishe kwamba usafi ni jambo la kwanza katika Wilaya yetu na ukilinganisha kwamba sisi ni Jiji Lazima tuendane na hadhi ya Jiji letu hivyo nipende kutoa shukrani zangu za dhati kwa kampuni zote zinazojihusisha na ukusanyaji wa taka ikiwemo Kajenjere Trading Company Limited kwani wanafanya kazi nzuri ya kuliweka Jiji letu katika hali ya usafi".
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.