Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Amos Makalla awaomba Wananchi wa Mtaa wa Mbondole Kata ya Msongola kuwa watulivu wakati Serikali yao sikivu ikitafuta muafaka na Mmiliki wa eneo lenye mgogoro katika Kata hiyo,hayo ameyabainisha leo May 9,2022 katika ziara yake ya kutatua mgogoro wa ardhi ambapo Wavamizi zaidi ya 700 walio uziwa ardhi ya Ndug. Martin Nasson kimakosa mpaka Sasa hawajui hatma yao Baada ya Mahakama kuamuru nyumba zaidi ya 200 za Wavamizi zivunjwe.
Aidha Katika mkutano wa Leo Mhe.Makalla kwa kushirikiana na Wataalamu wamepitia nakala zaidi ya 108 za mauziano ya zaidi ya Shilingi Milioni 179 ambapo kiasi chote hicho Cha fedha kimeliwa na wajanja wakiwemo Wajumbe wa mashina mbalimbali ya mtaa wa Mbondole hivyo Mhe.Makalla kuamuru kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mbondole na Wajumbe kwa tuhuma za kushiriki utapeli wa kuuza eneo la Mwananchi kwa Wavamizi zaidi ya 700 ambao mpaka Sasa hawajui hatma yao Baada ya Mahakama kuamuru nyumba zaidi ya 200 za Wavamizi zivunjwe.
Vilevile Mhe. Makalla ameelekeza wataalamu wa TAKUKURU kufanya mapitio ya Nyaraka zote za mauzioano ili ipatikane taarifa kamili na wote waliohusika wawajibishwe kwa mujibu wa sheria ambapo amekemea Vitendo vya uvamizi wa maeneo na uuzaji Ardhi kiholela.
Pamoja na hayo Mhe. Makalla amesema Baada ya kupatikana kwa taarifa kamili Serikali itakaa meza moja na Mmiliki, Wawakilishi wa Wavamizi na Kamati ili kupata muafaka wa pamoja wa kumaliza Mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 10 hivyo amewaomba wananchi wa mtaa wa Mbondole kusitishwa kwa Shughuli yoyote ya mauziano ya Ardhi na uendelezwaji wowote wa Ardhi mpaka pale Serikali itakapotoa maelekezo mengine.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.