Na; Mariam Hassan na Omary Omary
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Amos Makalla, leo tarehe 01 Septemba, 2021 amewaagiza Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Wakuu wa Shule za Sekondari za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanawaondoa Wafanyabiashara wote wanaofanya biashara holela pembezoni mwa maeneo ya shule zao.Agizo hilo amelitoa akiwa kwenye viwanja vya Buguruni Ghana katika Mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za Wananchi wa Jimbo la Segerea, ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya kusikiliza na kuzipatia majibu kero za Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.Aidha, moja kati ya kero kubwa zilizowasilishwa na wakazi wa Kata ya Buguruni ni malalamiko ya ufanyaji wa biashara kandokando ya maeneo ya shule ya Buguruni Kisiwani ambapo biashara hizo zimepelekea kuongezeka kwa uchafuzi maeneo yanayozunguka Shule hiyo pamoja na kuhatarisha usalama wa Shule na Mali zake, lakini pia Wanafunzi wanapoteza umakini wa kusoma kwa kuzunguka kwenye vibanda vya biashara kununua vitu wakati masomo yakiendeleaAkitatua kero hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema “hili naomba niliseme Mimi sijaridhishwa na hali hii katika shule zetu kwani hata shule ya Msingi Bunge wafanyabiashara,wanafanya biashara mpaka eneo la getini mwa shule hiyo mpaka mabanda yameizunguka shule hii inahatarisha usalama na kuwarubuni watoto wetu”.Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa amewaagiza wafanyabiashara wote wanaofanya biashara pembezeni mwa barabara ikiwemo maeneo ya Msimbazi, Kariakoo na pembezoni mwa barabara za mwendokasi, Kivukoni pamoja na maeneo mengine ambayo siyo rasmi kwa ajili ya ufanyaji wa biashara waweze kuondoka.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.