Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Paul Makonda ameeleza kwamba matumizi ya rasilimali za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni chachu ya uwajibikaji na upatikanaji wa taarifa sahihi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ya kimkakati jijini Dar es Salaam.
Makonda ameeleza hayo leo, Januari 15, 2020 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam wakati akizindua mfumo wa uratibu na usimamizi wa miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Dar es Salaam.
RC Makonda aliendelea kueleza kwamba mwaka 2020 jumla ya miradi 57 iliyopo katika ilani ya CCM lakini bado haijatekelezwa na mingine mipya inakuja kwa ajili ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kufikisha huduma na kuleta maendeleo kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.
Aidha RC Makonda amebainisha kuwa mfumo huu unawezesha uongozi, wasimamizi wa miradi pamoja na Idara husika katika ngazi zote kupata taarifa sahihi za maendeleo ya mradi kwa njia ya kidigitali na kurahisisha utoaji wa maamuzi sahihi na maelekezo pale inapohitajika.
"Kwa ujumla mfumo huu utaongeza uwazi, uwajibikaji, tija, miradi kukamilika kwa wakati na thamani ya fedha zinazotumika kwa mradi husika", alisema Makonda.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.