Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Bi. Tabu Shaibu ameishauri Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania TARI iweze kuandaa Mpango endelevu wa taarifa za tafiti ili ziweze kuwafikia walengwa na kunufaika na tafiti hizo za kilimo.
Hayo ameyasema Leo Desemba 4, 2024 Mkoani Dar es salaam wakati akifungua Mkutano uliowakutanisha Watafiti na Wadau wa Kilimo kwa lengo la kuuhabarisha Umma kuhusu mbegu Bora 19 mpya zilizofanyiwa Tafiti na TARI.
Bi. Tabu amesema Serikali inaendelea kuhakikisha Sekta ya kilimo inapiga hatua kwa mustakabali wa Taifa na Uchumi wa Watanzania ambapo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anahakikisha tafiti za mbegu za kilimo zinafanyika hapa Nchini ili ziweze kupunguza gharama.
"Serikali hawezi kuajiri Watanzania wote hivyo imeweka Mazingira wezeshi ya kuhakikisha Watanzania wanajiikwamua kiuchumi hivyo Vijana kupitia tafiti zilizofanywa na TARI wajiunge vikundi ili wapate mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri waweze kupata mitaji". Alisema Bi. Tabu.
Wakati huo huo, amewataka Wakulima waweze kuwa tayari kufuata maelekezo watakayopewa na Watalaam kuhusiana na mbegu hizo bora ili zikawape manufaa katika kilimo na Jamii Kwa Ujumla.
Kwa Upande wake Mtafiti Mwandamizi katika kituo Cha Utafiti TARI Tengeru Emmanuel Laswai amesema Kuna mbegu mpya ikiwemo za nyanya, pilipili hoho pilipili mbuzi na kichaa hivyo mbegu izo zinaweza kuoteshwa katika Mazingira ya kawaida na kustahamili magonjwa yatokanayo na mimea.
"Wakulima wakae mkao wa kula kwani mbegu hizi ni Bora na za uhakika ambazo zinastahamili ukame kwani zipo katika hatua za mwisho wa majaribio hivyo zitauzwa Kwa bei nafuu". Alisema Laswai.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.