Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas, akiongozana na Mkurugenzi msaidizi wa miundombinu ya TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Bw. Baltazar Kibola amekagua mafunzo kazi yanayotolewa kwa Maofisa Habari na Maafisa TEHAMA kutoka mikoa na Halmashauri za mikoa ya Dodoma, Singida, Iringa, Geita, Pwani, Manyara na Dar es Salaam yanayofanyika katika ukumbi wa Royal Village mkoani Dodoma.
Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Wakala ya Serikali Mtandao wamesanifu Mfumo wa pamoja utakaosaidia kutengeneza na kusimamia tovuti za Serikali ambazo zitakuwa na kiwango na muonekano mmoja ambao ni rahisi wakati wa kufanya maboresho.
Lengo la mafunzo kazi hayo ni kuwajengea uwezo Maofisa Habari na TEHAMA ili taarifa mbalimbali zinazohusu Serikali ziweze kuwafikia wananchi kwa usahihi na kwa wakati. Dkt. Hassan Abbas ameweka wazi sifa tano za Maofisa Habari na TEHAMA wa Serikali kwa nyakati hizi kuwa ni:
Dkt. Hassan Abbas amesisitiza kwamba Maafisa habari wa Serikali kote nchini moja ya vigezo vitakavyo tumika kuwapima katika utendaji wao wa kazi ni pamoja na upatikanaji wa taarifa mbalimbali zilizohuishwa katika tovuti zao.
Washiriki wa mafunzo hayo wameipongeza Serikali na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa kuwawezesha kupata ujuzi na stadi mpya za utengenezaji na uendeshaji wa tovuti za Serikali.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.