• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

USAFI KIPAUMBELE NAMBA MOJA CHA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM

Posted on: May 31st, 2021


Na.Rosetha Gange na Judith Damas

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makala leo Mei, 31 2021 amefanya kikao  kazi  na  Madiwani, wakuu wa idara, pamoja na watendaji kata  katika  ukumbi wa Arnatoglou uliopo  Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam  lengo kubwa likiwa ni kufahamiana na kuwaelekeza vipaumbele vyake akiwa ni  Mkuu mpya  wa Mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo usafi,utekelezaji wa ilani ya Chama, kutatua kero za wananchi,utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo,kuwapanga wamachinga pamoja na ulinzi na usalama.

Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Mhe. Makala ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kupata hati safi mara sita (6) mfululizo pamoja na kuwa vinara wazuri katika ukusanyaji wa mapato. Sambamba na hilo amewapongeza madiwani kwa kuwa wasimamizi wazuri katika kuhakikisha asilimia 10% ya  pato la ndani ya Halmashauri inatengwa kwa ajili ya  kuwawezesha wanawake, vijana na  watu wenye ulemavu kupata mikopo .

Aidha, Mhe. Makala amesisitiza suala la usafi katika Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwani hali ya usafi katika Jiji hili hairidhishi  hivyo amewataka watumishi pamoja na watendaji wa Kata kupanga mikakati ya haraka ili kulirejesha Jiji katika mandhari ya usafi kwani ndio kitovu cha wageni katika nchi yetu ya Tanzania.

“Jiji la Dar es salaam ni Jiji kubwa,watu mbalimbali wanafika hapa,Kwa hali ilivyo sasa hali si nzuri.Sijaridhishwa na hali ya usafi katika jiji la Dar es Salaam kwani hapa ndio uso wa Tanzania.Lazima jitihada za haraka zifanyike.”

Katika kuhakikisha suala hili linatekelezeka Mh.Makala amekusudia kuzindua kampeni ya usafi katika jiji la Dar es salaam na kuwasisitizia watendaji wote wa jiji wakawe wasimamizi wa zoezi hili na kuwa usafi uanze kwenye kaya,mitaa, kata na katika Halmashauri ya jiji lao.

Sambamba na hilo Mhe. Makala amesema kuwa atakuja na mpango wa kuwapanga upya  wamachinga na wafanyabiashara ndogo ndogo katika jiji la Dar es salaam ili jiji liwe kwenye muonekano mzuri na liwe katika hali ya usafi. Pia amesisitiza  kuwa kutokuwa na usimamizi na ufuatiliaji madhubuti kunafanya jiji kuonekana katika hali ya uchafu  na wahalifu hutumia vibanda hivyo kama maficho yao wakati wa usiku.


Akitoa shukrani kwa niaba ya watendaji wote wa Jiji la Dar es Salaam Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam  Mh.Omary Kumbilamoto  alimpongeza Mh.Makala kwa hotuba nzuri na kuahidi kuyatekeleza yale yote aliyowaagiza na kumuhakikishia  ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake.


Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.