Na: Hashim Jumbe
UZINDUZI wa Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) ngazi ya Wilaya umefanyika siku ya leo, tarehe 10 Mei, 2021 kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuzindua mashindano yake katika viwanja vya Magereza vilivyopo Ukonga, huku mgeni rasmi akiwa Katibu Tawala Wilaya ya Ilala, Bi. Charangwa Makwiro aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala.
Mashindano hayo yanashirikisha timu kutoka kwenye Klasta Nne (4) za kimasomo ambazo ni Chanika, Ukonga, Kimanga na Gerezani, yatafanyika kwa Siku Tatu (3) katika viwanja hivyo kuanzia leo.
"Tutakuwa hapa kwa muda wa Siku Tatu (3) sasa hivi tuna wachezaji 480 kutoka Klasta zetu Nne (4) baada ya hapo tutapata timu itakaa kambini kwa muda wa Siku Kumi (10) kwa ajili ya kuandaa timu yetu ya Wilaya teyari kwa mashindano ya Mkoa" Mwl. Sipora Tenga Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam akieleza
Aidha, mashindano hayo yanashirikisha michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu (football) kwa wavulana na wasichana, mpira wa mikono (handball) kwa wavulana na wasichana, mpira wa pete (netball) riadha kwa wavulana na wasichana, mpira wa viziwi 'goalball' mpira wa wavu (volleyball) wavulana na wasichana na pia mpira wa miguu wavulana kundi maalum (viziwi)
Itakumbukwa kuwa timu ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ni Mabingwa mara Nne (4) mfululizo wa mashindano ya UMITASHUMTA kwa ngazi ya Mkoa wa Dar es Salaam, na mwaka huu wa 2021 wamejipanga kushinda tena ushindi wa jumla wa Mkoa wa Dar es Salaam "tunategemea kufanya vizuri, sababu tumejiandaa kufanya vizuri, tumeanzia kutafuta wachezaji kuanzia shuleni tukaja kuwachezesha kwenye Kata, alafu Kata zikachagua wachezaji wazuri wakaja kwenye Klasta na hapa tuna Klasta Nne (4) ambazo zitashindana kutengeneza timu ya Wilaya ambayo itakwenda kushindana ngazi ya Mkoa" alisema Mwl. Tenga
Naye mgeni rasmi wa uzinduzi wa mashindano hayo Bi. Charangwa Makwiro ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala aliwaasa wanamichezo kuwa na nidhamu nakufuata maelekezo watakayokuwa wanapewa na kisha akawakumbusha mambo matatu ya kuzingatia "Sisi Wilaya ya Ilala tunakuwa na mambo matatu tu, huwa tunashinda, huwa tunaongoza na kuwa mfano kwa Wilaya nyengine, siyo kwenye michezo tu na hata kwa taaluma, kwa hiyo niwaombe katika hii michezo mfanye kwa bidii ili tuende kuinyanyua Ilala yetu"
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.