Mkuu wa Wilaya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewahakikisha Wajasiriamali Wilaya ya Ilala kuwapa ushirikiano pale wanapohitaji ili kukuza Masoko ya Wajasiriamali hao.
Amebainisha hayo leo Machi 09, 2023 wakati akifungua Semina ya Mpango wa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa ngazi ya Halmashauri iliyofanyika katika Ukumbi wa Arnatoglou Jijini Dar es Salaam, Semina hiyo iliwezeshwa na taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo TRA, TIRDO, TCCIA, BRELLA, TANTRADE na TBS.
Akifungua mafunzo hayo Mhe.Mpogolo Amesema “Mafunzo haya ni adhimu sana kwa wajasiriamali kwani suku hii ya leo watapata mafunzo haya yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kutafuta Masoko baada ya kuweka bidhaa zao Barcodes ambayo itawasaidia kuuza bidhaa hizo kwenye masoko rasmi hivyo niwaombe Wajasiriamali msikilize kwa makini na muende mkaishi haya yote mnayoelekezwa.”
Kwa upande mwingine Mhe. Mpogolo aliweza kuzindua kampeni ya GS1 Tanzania Barcode day itakayoanza June 15-19, 2023 yenye kauli mbiu isemayo ‘GS1Tanzania beyond Barcode’ ambapo aliweza kuwasisitiza wajasiriamali kujitokeza kwa wingi, “Ili kuwakomboa kina mama lazima kina mama muungane na mimi niwahakikishieni kwenye hiyo kampeni ya Kata kwa Kata nitakuwepo kwani tutafanya kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ambaye nia yake ni kuwakomboa wananchi kiuchumi hususani Wanawake hivyo nawapongeza GS1 na timu nzima kwa kampeni hizi naamini kila Mjasiriamali wa Wilaya ya Ilala atanufaika na fursa hii.”
Naye Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salam Bi. Tabu Shaibu awashukuru GS1 kuandaa semina ya mafunzo kwa Wajasiriamali ambayo itawasaidia kupata uelewa jinsi ya kuboresha bidhaa zao ili ziwe na viwango na ubora na kuweza kukidhi Soko la ushindani ambapo zitaweza kukuwa na kufikia Soko la kimataifa.
Aidha, kwa upande wake mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu amemuhakikishia Mkuu wa Wilya kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Kitengo chake cha Maendeleo ya Jamii iko tayari kuyafanyia kazi yale yote yaliyoelekezwa kwenye semina hiyo ili kuinua Wajasiriamali hao.Pia awataka Wajasiriamali kusikiliza kwa makini semina hiyo ya mafunzo ili kutoka na uelewa jinsi gani ya kuboresha bidhaa zao.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Bi. Kange Ameeleza kuwa “Baada ya Wajasiriamali kuonekana wanazalisha bidhaa bora lakini hazina msimbomilia(BARCODE) Ofisi ya Rais TAMISEMI wakaona ni vyema kutoa kibali kwa Taasisi ya GS1 ambao ndio hutengeneza Barcodes kuandaa mafunzo katika kila Halmashauri nchini ya kuwafundisha Wajasiriamali umuhimu wa Barcodes ambapo kila Halmshauri iliweza kuingia makubaliano ya mafunzo hayo kwa kuchangia Shilingi Milioni 5 zakuwezesha mafunzo hayo hivyo mafunzo haya ya kuwajengea uwezo Wajasiriamali juu ya umuhimu na matumizi ya msimbomilia (BARCODES) yameanza kufanyika leo kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambapo vikundi Vitano (5) Vitaweza kuchaguliwa."
Sambamba na hilo Bi. Kange ameeleza kuwa baada ya mafunzo wataweza kuwasaidia wafanyabiashara kutafuta masoko kwani kuna masoko Canada na Marekani ila masoko haya yatahudhuriwa na vikundi ambavyo vitaweza kukidhi vigezo na pia vitakavyotengeneza bidhaa bora na zenye viwango
Aidha Bi.Kange ameendelea kusema “Sisi kama wajasiriamali tuhakikishe tunatengeneza bidhaa kwa kiwango na pia tunaweka mifumo kupitia Maafisa Maendeleo wa Halmashauri ya Jijj la Dar es Salaam huku tukipanga kiwango cha pamoja cha kuuza bidhaa zetu hivyo niwasisitize mtengeneze kurasa za mitandao ya kijamii kwaajili ya kutafuta masoko rasmi.”
Vilevile Bi.Kange amshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kufungua mipaka ambayo ni fursa kwa wananchi wa Tanzania, “Naamini sisi kama wajasiriamali tutatumia fursa hii ya mheshimiwa Rais wetu hivyo sisi GS1 tutashirikiana na wajasiriamali kupata masoko nje ya nchi ya Tanzania hivyo tutahakikisha tunawaelekeza namna ya kutengenezea kurasa katika mitandao ya kijamii na namna gani mnaweza kupata masoko.”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.