Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imetoa Mafunzo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu vitakavyopatiwa mkopo kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023. Mafunzo hayo yataendeshwa kwa siku tatu mfululizo, na yameanza na Jimbo la Ilala ambapo Ukonga na Segerea zitafuata.
Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Eng. Amani Mafuru leo tarehe 01 Februari, 2023 katika Ukumbi wa Arnatoglou, Dar es Salaam amewataka Wajasiriamali hao kuzingatia mafunzo hayo na kuyafanyia kazi ili waweze kusimamia miradi kwa weledi na kuweza kurejesha marejesho kwa wakati.
Aidha Eng. Mafuru amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muugnano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuweza kusimamia utekelezaji wa kuwezesha wananchi kiuchumi kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya kila Halmashauri nchini inayowezesha kupatikana kwa fedha hizo za mikopo pamoja na Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kusimamia vyema zoezi hili.
Kaimu Mkurugenzi ameeleza kuwa Halmashauri ina imani kuwa baada ya vikundi kupatiwa mikopo hiyo vitaweza kukuza uchumi binafsi na kwa maendeleo ya Taifa.
Naye, Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi. Margareth Mazwile ameeleza kuwa semina hii imewajumuisha wanavikundi 150, ambavyo vikundi 27 kutoka Jimbo la Ilala vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu wamejifunza mada zifuatazo; Masuala ya Uongozi, Usimamizi wa Fedha na Masoko, Uendeshaji wa Mradi, Utoaji wa Taarifa na Utunzaji na Ujazaji wa Nyaraka muhimu za Kikundi na taratibu zinazohusu mkopo ambapo mada hizo zina Lengo ya kuwapatia walengwa ujuzi wa taaluma katika maeneo yafuatayo ; Elimu ya Ujasiriamali, Kujua mbinu za kutafuta Masoko, Utunzaji kumbukumbuku na nyaraka za biashara na Kufahamu faida halisi katika biashara.
Aidha, Mwenyekiti wa kikundi cha Mahanjumati Bi. Jokha Lemky ameishukuru Serikali kwa kuwawezesha kiuchumi kupitia mikopo ya 10% ya Mapato ya Ndani na kuahidi kurejesha kwa wakati ili wananchi wengine waweze kupata mikopo hiyo na kuviasa vikundi vingine viweze kuzingatia waliyofundishwa na kuweza kutimiza lengo la Serikali kuwawezesha wananchi kukua kiuchumi kwa kuwapa mikopo wananchi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.