Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Tanzania Interfaith Partinership (TIP), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndaki ya TEHAMA pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto UNICEF leo tarehe 09 Novemba, 2023 wameendelea na mafunzo Katika Tarafa ya Segerea juu ya ugharibishaji wa hamasa ya huduma za chanjo kwa wahudumu wa afya ngozi jamii kwaajili ya watoto chini ya miaka mitano katika Jiji la Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Comfort uliopo Tabata Shule Jijini Dar es Salaam yaliwajumuisha Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Maafisa Afya wa Kata pamoja na watoa huduma za afya ngazi ya jamii wa Tarafa ya Segerea.
Akiongea wakati wa Mafunzo hayo Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndaki ya TEHAMA Dkt. Hellen Maziku ameeleza kuwa “Kupitia mpango wa uwezeshaji jamii kutambua changamoto za kiafya na kuweka mikakati ya kukubaliana na changamoto hizo (HCD) tumeweza kuwahudisha wananchi moja kwa moja ili kujua tatizo ni nini katika kutekeleza afua zetu hivyo leo tumefanya mafunzo katika Tarafa ya Segerea kuwaeleza juu ya umuhimu wa chanjo kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano pamoja na kutoa maelekezo kwa watendaji hawa ambao wataenda kusimamia zoezi hili litakaloanza siku ya jumatatu tarehe 13 Novemba, 2023 ambapo kila mtoa huduma wa afya ngazi ya Kata atatakiwa kufikia nyumba 40 kwa siku na baada ya hapo naamini tutakua tumefika lengo.”
Sambamba na hilo Dkt. Maziku ameeleza kuwa baada ya kumaliza zoezi hili wataalamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili watafanya tathmini ya zoezi zima kama limefanikiwa kwa kiwango gani.
Naye Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Jimbo la Segerea George Mtambalike ametoa wito kwa Wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hili kwani chanjo ni muhimu kwa watoto na haina madhara yoyote hivyo watot ushirikiano ili zoezi liweze kufanikiwa kwa asiliia 100% katika Tarafa yetu ya Segerea na Halmashauri kwa ujumla.
Zoezi hili linatarajiwa kuanza Novemba 13, 2023 katika Jimbo la Segerea mitaa ya Segerea, Kisukuru, Kimanga, Liwiti, Kipawa, Kiwalani pamoja na Minazi Mirefu itafikiwa kwa siku tano huku mitaa ya Kinyerezi, Bonyokwa, Mnyamani, Vingunguti, Tabata, pamoja na Buguruni ikifikiwa kwa siku kumi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.