• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Wajumbe wa Halmashauri Kuu wapitisha Taarifa Ya Utekelezaji Wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Halmashauri ya Jiji la DSM

Posted on: September 6th, 2024

Katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  leo Septemba 06, 2024 Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala imepokea Taarifa ya Utekelezaji wa miradi iliyotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuanzia Januari - Juni 2023.

Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Arnatouglou Jijini DSM na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala, Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala, Mkuu wa Wilaya wa hiyo, Wajumbe wa Halmashauri Kuu Wilaya ya Ilala pamoja na Watumishi kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala Ndg. Alhaji Said Sidde amesema “Niwapongeze Wajumbe wa Halmashauri Kuu kwa kupokea na kupitisha Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pia nipende kuipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kutekeleza Ilani ya Chama kwani wameweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuboresha huduma za wananchi. Niwaombe viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha mnatekeleza yale yote tuliyowaelekeza wakati wa ziara yetu na pia muhakikishe miradi yote inatekelezwa kwa wakati uliopangwa pia niwaombe wajumbe kuhakikisha mnashiriki kikamilifu kujiandikisha kupiga kura kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwabkufanyika Novemba 27, 2024."

Akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala  Mhe. Edward Mpogolo ameeleza kuwa katika kuimarisha hali ya ulinzi na usalama Wilaya inaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala kwa kuhakikisha Ilala ipo Shwari.

Aidha Mhe. Mpogolo ameendelea kusema “Katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Idara zake zikiwemo Idara ya Elimu, Idara ya Afya pamoja na  Idara ya Maendeleo ya Jamii ambapo katika Idara ya Elimu Msingi na Sekondari, Halmashauri ya Jiji la DSM imeendelea kuboresha miundombinu ya shule za msingi kwa kipindi cha miaka minne ambapo zaidi ya bilioni 7 fedha kutoka mradi wa Boost, EP4R na mapato ya ndani ya Halmashauri zikitolewa kutekeleza miradi ya ujenzi wa madarasa Elimu msingi pamoja na uboreshaji wa miundombinu huku kwa upande wa Elimu Sekondari kwa kipindi cha miaka minne Halmashauri imeweza kujenga shule nane za ghorofa zikiwa na madarasa 20 pamoja na matundu 45 ya vyoo ambazo zimekua chachu ya kupunguza msongamano wa wanafunzi mashuleni huku Halmashauri ikiwa na mkakati wa kujenga maghorofa mengine 10 ya namna hiyohiyo,utekelezaji wa wa miradi hii umetokana na fedha kutoka Gharama za mpango wa Elimu bila malipo, Serikali Kuu, Mapato ya Ndani ya Halmashauri na wafadhili, SEQUIP na BARRICK. Pia miundombinu ya Afya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa  kipindi cha miaka minne imepokea kiasi cha zaidi ya bilioni 100  zikiwa ni za ukarabati wa miundombinu chakavu, Ujenzi wa vituo tisa vya Afya ambapo vituo saba vimekamilika na vituo viwili vikiwa katika hatua za mwisho, ujenzi wa hospital na ununuzi wa vifaa tiba ikiwemo mashine za kisasa halikadhalika idara hiyo imepokea magari ya kubebea wagonjwa takribani 6, magari manne yakiwa yamepokelewa kutoka Serikali kuu na magari mawili yakinunuliwa kwa fedha za mapato ya ndani hivyo kuleta jumla ya magari 12 ya kubebea wagonjwa. Kwa upande wa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Jiji kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imefanya uhamasishaji na kutoa mikopo kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ambapo Halmashauri imeweza kutoa kiasi cha Tsh bilion 17. 2 kwa vikundi 1462 aidha idara hiyo imeweza kuwatambua vijana elfu 12 wa bodaboda lengo likiwa ni kuhakikisha wanatambua vituo vyao ili vijana hao wa Bodaboda waweze kuvaa vazi rasmi na pindi fursa za mkopo wa asilimi 10% vijanaa hao waweze kupata, vilevile idara hiyo imeendelea kuunga mkono matumizi ya Nishati safi ya kupikia ambapo zaid ya mama lishe elfu moja wametambuliwa na baadhi yao wameweza kupewa majiko.”

Katika hatua nyingine, Mhe. Mpogolo ameeleza kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeweka mipango endelevu ya kujenga masoko ya kisasa yatakayowasaidia wananchi kujipatia kipato na Jiji kuendelea kupata mapato

Sambamba na hilo Mhe. Mpogolo ameendelea kusema “Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya Wilaya ya Ilala, pia ameweza kuishukuru Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya kwa kushirikiana na Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha tunatekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi hivyo nikuahidi miradi mingine ambayo haijakamilika inaenda kukamilika kwa wakati na pia nikuhakikishie tutaenda kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wananchi kwa kuhakikisha wanafahamu maendeleo yaliyofanyika na serikali yetu kwa miaka mitano pia nikuhakikishie kwenda kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kujiandikisha na kushiriki kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27,Novemba 2024”.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndg. Elihuruma Mabelya ameeleza kuwa “Nipende kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha za utekelezaji wa miradi kwa Halmashauri yetu kwani Sisi kama Halmashauri mipango yetu inaongozwa na Ilani ya CCM katika yale yote tunayoyatekeleza kwenye Kata na mitaa yetu kama uboreshaji wa miundo mbinu mbalimbali ya Afya , elimu na barabara hivyo niombe ushirikiano wenu kama Halmashauri Kuu ya Wilaya kuhakikisha Ilani ya Chama inatekelezwa katika Halmashauri yetu na nipo tayari kupokea maelekezo nitakayopewa”.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.