Diwani wa Kata ya Jangwani Mhe. Zacharia Digosi amewapongeza walimu wa Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja kwa juhudi wanazozifanya ikiwa ni pamoja na kuongeza ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha pili kwa mwaka 2023.
Pongezi hizo zimetolewa Leo tarehe 26 Januari, 2024 wakati wa halfa fupi ya kuwapongeza wanafunzi wa kidato cha pili waliofanya vizuri kwenye upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili 2023, iliyofanyika katika shule hiyo iliyopo Wilaya ya Ilala Jijini DSM.
Akiongea na wanafunzi, walimu pamoja na wazazi/ walezi Mhe. Digosi amesema "Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi wa shule. Pia nawapongeza walimu kwa jitihada zao kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu iliyokusudiwa, ufaulu umeongezeka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka iliyopita, hivyo walimu wanasikiliza na kutekeleza ushauri na maoni kutoka kwa viongozi na wazazi, ni kazi ngumu lakini hawakati tamaa, wazazi pia tusiache kufatilia maendeleo ya watoto wetu shuleni.”
Sambamba na hilo Afisa Elimu Taaluma Sekondari Bi. Rozina Salema ambaye pia ni mlezi wa shule hiyo, amesema "Nawapongeza wanafunzi wote waliofanya vizuri, pia walioshindwa wasikate tamaa wana nafasi nyingine niwatie moyo mkazane kusoma kwa bidii mtimize ndoto zenu.”
Awali akifungua halfa hiyo Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Joram Elly Nkya amemshukuru Mhe. Digosi kwa kushiriki katika halfa hiyo, pia amesema halfa hii iwe chachu kwa wanafunzi wengine kufanya vizuri katika masomo na mitihani yao.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.