Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI (ELIMU) Mhe. Zainab Katimba ametoa rai kwa Watumishi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa wanaoshiriki mashindano ya SHIMISEMITA 2025 kutumia fursa ya mashindano hayo kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la upigaji kura wa kuchagua Rais Wabunge na Madiwani siku ya Oktoba 29, 2025.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa mashindao hayo mapema Agosti 23, 2025 katika Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga Mhe. Katimba amewataka watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kushiriki kikamilifu mashindano haya na kuwakumbusha wananchi kuhusu zoezi kubwa la kitaifa la uchaguzi ikiwa ni sambamba na kiwaeleimisha wananchi hao juu ya faida ya kuchagua viongozi bora kwa maendeleo ya michezo na taifa kwa ujumla.
“Kupitia kauli mbiu hiyo Sanaa na Michezo ikawe chachu ya watumishi wengine ambao hawakupata fursa hii na jamii kwa ujumla kuonesha uzalendo wa kuipenda nchi yao kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, 2025 na kuchagua viongozi walio bora na siyo bora viongozi” amesema Mhe. Katimba.
Aidha, Mhe. Katimba ametumia fursa hii kuwataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa nchini kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya kuwezesha michezo
Ikiwemo migao ya kila mwezi katika Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa ili iwasaidie katika kuratibu shughuli za michezo sambamba na ushiriki wa wanamichezo kutoka kwenye kila Halmashauri husika kwani michezo inasaidia kuimarisha afya, ukakamavu, upendo, ushirikiano pamoja na kudumisha nidhamu mahala pa kazi.
Katika Hotuba yake Mhe. Katimba amethibitisha kuwa jumla ya Halmashauri 150 kati ya 184 zimeshiriki Mashindano ya SHIMISEMITA 2025 ambapo jumla ua watumishi 3504 wamewasili Jijini Tanga huku miongoni mwao Wanaume wakiwa 2114 na Wanawake 1390.
Sambamba na hilo Naibu Waziri Mhe. Katimba amesisitiza na kuelekeza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinashiriki kikamilifu mashindano yajayo ya SHIMISEMITA mwaka 2026.
Mashindano haya ya SHIMISEMITA 2025 yenye kauli mbiu ya “Jitokeze Kupiga Kura kwa Maendeleo ya Michezo” yanaendelea hapa Jijini Tanga ambapo wanamichezo kutoka Halmashauri 150 nchini wanashiriki.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.