Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewataka Wananchi kuhakikisha wanasimamia ulinzi na usalama katika maeneo yao kwani ndio msingi wa maendeleo ya jamii katika ngazi zote, na hakuna jamii ambayo itajivunia kupata muelekeo wa maendeleo kama kwao usalama haupo.
Mhe. Mpogolo ametoa rai hiyo leo Septemba 19, 2024 wakati akifanya Mkutano na viongozi wa Chama na Serikali wa Jimbo la Ilala, uliofanyika katika ukumbi wa Drimp wenye lengo la kutoa elimu kwa viongozi hao kuwa na mahusiano mazuri na kuendelea kushirikiana katika kuhakikisha Ilani ya Chama inatekelezwa na huduma za kijamii zinaboreshwa kwa wananchi.
Aidha, Mhe. Mpogolo amewasihi wananchi kuhakikisha kila mmoja anakua mlinzi wa mwingine katika kuhakikisha wanakemea vitendo viovu vinavyoendelea katika Jamii na kuhakikisha wanashirikiana na Jeshi la polisi kutoa taarifa pindi watakapoona watu ambao hawawaelewi katika maeneo yao.
“Niwajibu wetu kuunga mkono Serikali kwa kusimamia amani na usalama wa nchi yetu kwani Wawekezaji wanakuja kuwekeza nchini kwetu kwasababu kuna amani bila amani wawekezaji hawawezi kuwekeza nchi hivyo tutoe taarifa kwa Jeshi la polisi pindi tunapowaona watu tusiowaelewa katika maeneo yetu wanaoonekana kuleta uvunjifu wa amani hii itasaidia kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo katika mitaa yetu”. Amesisitiza Mhe. Mpogolo.
Halikadhalika, Mhe.Mpogolo amewasihi viongozi kuhakikisha wanashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kuwahamasisha Wananchi kujiandikisha katika daftari la makazi ili kuweza kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27, 2024 huku akiwasihi Wananchi wenye sifa za kugombea kujitokeza kuchukua fomu ili waweze kugombea kwa maendeleo ya wananchi na Jiji kwa ujumla.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.