Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji leo tarehe 23 Agosti, 2024 wamefanya ziara katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika eneo la ukusanyaji wa mapato pamoja na utekelezaji wa miradi.
Wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Arnatoglou Jijini humo, Wataalumu hao waliweza kujifunza namna mbalilimbali Jiji la Dar es Salaam linavyofanya kazi zake katika eneo la ukusanyaji wa mapato pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali za kuongeza mapato pamoja na kusimamia miradi kwani kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mapato yameongezeka kwa kasi kutokana na kuanzishwa kwa kanda za huduma ambazo zimekua chachu ya ongezeko la asimia 105% ya mapato ya ndani ya Halmashauri ukilinganisha na mwaka 2022/2023.
Akiongea wakati wa Mafunzo, hayo Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndg. Elihuruma Mabelya ameeleza kuwa “Napenda kushukuru ujio wenu kwani Ujumbe huu unaonesha jinsi gani Jiji la Dar es Salaam tumejiimarisha katika eneo la ukusanyaji wa Mapato hadi kuwa kivutio kwa wengine kujifunza kwetu hivyo kipekee napenda kutoa Shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa fedha anazoendelea kuzileta Jijini kwetu za utekelezaji wa Miradi pamoja na Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam ambao wao ndio wasimamizi wakuu wa miradi hii kwakua ni wenyeviti wa mabaraza ya maendeleo ya Kata wamekua wakishirikiana na Sisi pamoja na wataalamu wote kuhakikisha mapato yanaongezeka na miradi inatekelezwa kwa Wakati hii ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati hivyo niwaombe Wataalamu kutoka Rufiji mkatekeleze vyote mlivyojifunza bila kusahau ushirikiano na viongozi wenu hususani Madiwani kwao bila hao mafanikio hayawezi kuja kirahisi.”
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Bw. Sebastian Gaganija ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Uthibiti wa Taka Ngumu amempongeza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam pamoja na watendaji wote kwa kuweza kushirikiana vyema katika kukuza mapato ya Jiji pamoja na uaimamizi na utekelezaji mzuri wa miradi huku akiahidi kwenda kufanyia kazi yote waliyojifunza.
“Kwa hakika sisi kama Watendaji wa Halmashauri kwa niaba ya Mkurugenzi wetu na watendaji wote tunaishukuru sana Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ziara hii tumejifunza vya kutosha na tunaimani tumebadilishana uzoefu vya kutosha na kuweza kuyafanyia kazi tukirudi Rufiji. Pia Nachukua nafasi hii kuipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo ni chachu ya maendeleo kwa nchi yetu.” Amesema Bw. Gaganija.
Aidha, Wataalamu hao Waliweza kutembelea Soko la Kimataifa la Samaki Feri pamoja na Soko la Kisutu kujifunza namna Jiji la Dar es Salaam linavyoendesha masoko hayo katika kuhakikisha mapato yanaongezeka.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.