Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewataka viongozi kushirikiana na wazazi na walezi kutoa Elimu ya maadili kwa watoto, Rai hiyo ameitoa leo Septemba 18, 2024 kwenye muendelezo wa semina kwa Viongozi wa Mashina, Matawi, Mitaa na Kata wa Kata za Kimanga, Tabata na Liwiti lengo likiwa ni kumjenga mtoto katika maadili yanayofaa na kukubalika katika jamii.
“Viongozi tuwe wamoja kuwakemea vijana na wababa wanaoharibu watoto, na tukatoe Elimu kwa watoto ya mabadiliko na mahusiano ili kukwepa mimba za utotoni na maambukizi ya UKIMWI kwani takwimu zinaonesha kuwa watoto chini ya miaka 17 wana maambukizi ya Ugonjwa huo huku watoto wakike wakiwa wanaongoza hivyo inabidi ninyi kama viongozi mshirikiane na Wazazi na walezi katika kuwalinda na kuwalea watoto katika malezi mema ili kujenga kizazi bora na chenye maadili ambacho kitafuata mila na desturi za taifa letu”. Amesema Mhe. Mpogolo.
Sambamba na hilo, Mhe. Mpogolo amewataka wazazi kufuatilia mienendo ya watoto wao hasa waliomaliza darasa la saba hivi karibuni Ili wasije kujiingiza kwenye mahusiano na watu waliowazidi umri na kupelekea kupata mimba na kushindwa kurudi Shuleni.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.