Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. William Lukuvi (Mb) amewapongeza Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Ilala Kwa kusimamia Vizuri Mradi wa barabara ya Mtaa wa Tukuyu Jijini Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 0.62 uliogharimu zaidi ya shilingi milioni mia nane.
Waziri Lukuvi ameyasema hayo Oktoba 9, 2024 mara baada ya kukagua na kuzindua barabara hiyo Jijini humo ambapo amesema kukakamilika Kwa Mradi huo ni juhudi za Mheshmiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha anatatua changamoto zinazowakabili Wananchi hapa Nchini.
"Kukamilika Kwa barabara hii inakwenda leta tija na manufaa ya Wakazi wa Jimbo hili la Ilala na Taifa Kwa Ujumla hivyo barabara hii itaunganisha Mitaa mbalimbali ikiwemo Lindi na Moshi". Alisema Mhe. Lukuvi.
"Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi."
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.