• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Waziri Mchengerwa awataka viongozi kusimamia vizuri na kulinda maslahi ya Walimu na Watumishi wote

Posted on: November 27th, 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohammed Mchengerwa (Mb) amewataka viongozi wa Mikoa pamoja na Serikali za Mitaa kusimamia vizuri na kulinda maslahi ya Walimu na Watumishi wote Nchini wanaosimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya kukabidhi vitendea kazi vipya ikiwemo Gari Toyota Coaster Mini Bus moja (1), Pikipiki 62 pamoja na Kompyuta mpakato 159 kwa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Tambaza Jijini Dar es Salam.

Akiongea wakati wa hafla hiyo Mhe. Mchengerwa ameeleza kuwa “Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha sekta ya elimu nchini kwani zaidi ya shilingi bilioni 800 zimetumika kwaajili ya elimu bure hivyo kwa kutambua juhudi hizo inabidi tufanye kazi kwa bidii kwa kuhakikisha tunasimamia vyema miradi ya elimu ikamilike kwa wakati sambamba na kuhakikisha maslahi ya walimu yanazingatiwa na kulindwa kwani ili tutoe elimu bora lazima tutengeneze mazingira bora kwa walimu kwa kuzingatia misingi aliyotuachia Baba wa Taifa ya kuhakikisha tunapambana na adui watatu yani umaskini, maradhi na ujinga hivyo niwaagize TSC kufanya Mapitio kwa walimu wote wanaostahili kupanda vyeo ili waweze kupanda kwa wakati.”

Sambamba na hilo Mhe. Mchengerwa amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamia miradi yote inayotekelezwa katika Halmashauri zao ikiwemo ujenzi wa madarasa kukamilika kwa wakati na ikitokea hawajakamilisha hatua za kisheria zitachukuliwa huku akiendelea kuwasisitiza Wakurugenzi wa Halmashauri kupanga mipango ya maendeleo inayoendana na matumizi husika ambayo yanalenga wananchi hivyo vipaumbele vya maendeleo viwaguse wananchi moja kwa moja.

Awali Akitoa  Shukrani zake kwa Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa  kuboresha sekta ya elimu nchini Mkuu wa Wilaya  Mhe. Edward Mpogolo amesema “Kwa kipindi cha miaka miwili ya Rais wetu Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam tumepokea zaidi ya bilioni 20 kwaajili ya kuboresha miundombinu ya elimu pamoja na kuendesha elimu bure ambapo nasisi kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri tumeweza kutengeneza madawati elfu 20 kwa Shule za Msingi pamoja na viti na meza 17,600 kwa shule za Sekondari za Halmashauri ya Jiji na utekelezaji unaendelea hivyo nikuhakikishie Mheshimiwa Waziri tutaendelea kusimamia yale yote utakayotuelekeza kwa maslahi ya Wananchi wetu na Nchi kwa ujumla.”

Kwa upande wake Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Paulina Nkwama ameeleza kuwa shilingi milioni 454.6 fedha kutoka mradi wa boost zimetumika kununua vitendea kazi vilivyokabidhiwa kwa watendaji wa TSC nchini  ikiwemo  Pikipiki 62, gari moja kwaajili ya kazi za makao makuu, pamoja na kompyuta mpakato 159 ambapo 139 zitagawanywa katika wilaya zote Nchini huku 20 zikibaki kwa matumizi ya Makao makuu, hivyo kutoa shukrani zake kwa Rais na kumuhakikishia mpaka 2025 sekta ya elimu nchini itakuwa imeboreshwa zaidi.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.