• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Waziri Mhagama awataka TARURA kuimarisha Kivuko cha Mwanagati-Magole

Posted on: November 22nd, 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama (Mb), amewataka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) kuimarisha kivuko cha Mwanagati-Magole mara tu baada ya mvua kupungua.

Waziri Mhagama ameyasema hayo leo Novemba 22, 2023 alipokuwa akiongea na wananchi wa Mtaa wa Mwanagati na Magole katika ziara yake ya kufanya tathmini na ufuatiliaji wa maeneo yaliyoathiriwa na mvua kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo eneo mojawapo likiwa ni eneo la daraja linalounganisha Mitaa hiyo ya Kata ya Mzinga Jijini Dar es Salaam.

“Agizo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha miundombinu yote yahuduma kutoa huduma kwa wananchi wa Tanzania na ndio maana kutokana na umakini wa Serikali yetu leo tumefika mahali hapa kujionea wenyewe adha wanayoipata wananchi wa Kata ya Mzinga hivyo tumetoa shilingi milioni 20 kwa ajili ya TARURA kuimarisha kivuko hiki hivyo niwaombe wataalamu kutoka TARURA mara tu baada ya mvua kupungua kivuko hiki kiimarishwe ili wananchi waweze kupita muda wote huku mipango ya kujenga kivuko cha muda mrefu ikiendelea kufanyika kwani mvua zikiisha kivuko cha muda mrefu kitaaza utekelezaji, pia nitoe angalizo fedha hizi zitumike ipasavyo isitokee mtu yoyote kuweka mfukoni mwake kwani hatua za kisheria zitachukuliwa na pindi tu mtakapoanza ujenzi  wananchi washirikishwe kwa ukaribu zaidi katika hili,” Amesema Mhe. Mhagama.

Akiendelea kuongea na wananchi wa Kata ya Mzinga Mhe. Mhagama ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kipindi hichi cha mvua hasa wale wanaoishi karibu na mikondo ya maji huku akiwasisitiza kutunza mazingira kwa kuyaweka katika hali ya usafi ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko kama Kipindupindu ambayo hutokea kipindi hiki cha mvua.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila ameema “Tunaishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuja kuona hali halisi ya namna ilivyo lakini nipende kuwaambia mpaka sasa Dar es Salaam hakuna mafuriko bali kwa wananchi wa Mzinga adha yao kubwa ni miundombinu ya Daraja pamoja na miundombinu ya barabara ambayo imeharibiwa na mvua hivyo niwahakikishie adha hii inakwenda kuisha kwani tayari TARURA wameshachora mchoro wa kujenga daraja hili ambao utagharimu shilingi bilioni 1.7 lakini pia kwa upande wa barabara DMDP awamu ya pili barabara hii imeingia kwenye mradi huu hivyo itatengenezwa barabara ya kiwango cha lami yenye KM 7 itakayoka kwa Mpalange Mpaka kuunganisha barabara ya Mwanagati inayopitia Banana hivyo niwaombe mume wavumilivu kwani kero zenu tumezisikia na tunazifanyia kazi.”

Awali akiongea wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo Ametoa shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuhakikisha Wananchi wanapata huduma kwa wakati huku akimuhakikishia Waziri Mhagama kusimamia kwa ukaribu zaidi yote atakayoyaelekeza.


Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.