Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka Maafisa habari kutumia vyema elimu na uzoefu walionao kutoa taarifa sahihi kwa wakati hasa kwa Serikali na Viongozi wetu huku akiwataka watekeleza wajibu wao katika kutimiza majukumu yao ya kutoa taarifa kwa Wananchi.
Waziri Majaliwa ameyasema hayo leo Mchi 27, 2023 wakati akifungua Kikao kazi cha 18 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serekalia kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere International Conventional Centre (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Aidha Waziri Majaliwa ametoa wito kwa Maafisa Habari kuongeza ubunifu ili kusukuma agenda za Serikali kuwafikia wananchi. “Ndugu wanahabari hakikisheni mnafanya kazi ya kutoa habari sahihi kwa ukamilifu na kwa wakati ili wananchi waweze kufikiwa na habari hizo kwani Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatambua mchango mkubwa mnaoufanya katika kuchochea miradi mbalimbali na hatowaangusha atashirikiana na nyinyi bega kwa bega kuhakikisha sekta hii ya habari inasimama imara.
Vilevile Waziri Majaliwa ameendelea kusema “Ni matumaini yangu mtatoa taarifa za utekelezaji wa miradi kwa wananchi hivyo niwahakikishie kwamba Serikali inatambua mchango wenu na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia baada ya kikao hichi tasnia hii itaenda kufanya mabadiliko makubwa katika utoaji wa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya nchi yetu kwa wananchi.”
Sambamba na Ufunguzi huo Mhe. Waziri Mkuu aliweza kupokea tuzo ya heshima kwaajili ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika kukuza tasnia ya habari nchini pia aliweza kuzindua jarida la ‘Nchi yetu’ linaloeleza mafanikio ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha uongozi wa miaka miwiliya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wake Waziri wa Habari,mawasiliano na Teknolojia ya habari Mhe. Nape Nauye ameeleza kuwa “Nashukuru sana Jitihada za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa sekta ya habari pamoja na kudumisha Demokrasia nchini kwani aliweza kuhudhuria mkutano wa hadhara kwa Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo hivyo ni imani yangu kikao hichi kitawajengea uwezo katika kusukuma maendeleo ya nchi yetu.”
Sambamba na hilo Mhe. Nnauye amekitaka Chama cha TAGCO kutekeleza majukumu yake bila kujitegemea hivyo baada ya kikao hichi Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari itasimamia na kuratibu mambo yote ya maafisa habari, mawasiliano na uhusiano Serekalini.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Selestine Gervas Kakele amesema “Katika Kikao kazi hichi cha 18 Kutakua na mada mbalimbali zitakazo tolewa kwa Maafisa habari wetu ambapo kutakua na mada ya kujifunza jinsi ya kuhariri habari, mada kuhusu uboreshaji na utunzaji wa Mazingira, Wajibu wa Maafisa habari katika uchaguzi wa viongozi wa Nchi yetu."
Sambamba na hilo Bw. Kakele Ameeendelea kusema baada ya kikao hichi matarajio yetu ni kuwa maafisa habari hawa watakua wamejengewa uwezo wa kutoa taarifa zinazolinda taasisi zao, maarifa ya kupata taarifa Sahihi kwa wakati kwa vyanzo husika, kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi pamoja na kuwahoji wananchi kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili katika kuendelea kuwaletea maendeleo na kuzifikisha sehemu husika ili ziweze kutatuliwa.
Aidha katika Kikao kazi hicho cha 18 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali chenye kauli mbiu isemayo ‘MAWASILIANO YA KIMKAKATI INJINI YA MAENDELEO’ kimeweza kubeba sura ya umuhimu wa sekta ya habari katika kuchochea maendeleo kwa wananchi wake huku wakiweza kutambua na kutekeleza Agenda za Kitaifa ambapo itawajengea uwezo wa kueleza vizuri na kwa ufasaha miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Nchini Tanzania kiliweza kuhudhuriwa na Maafisa Habari takribani 600 Kutoka Wizara, Taasisi Mbalimbali na Halmashauri zote Nchini, Maafisa habari kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wadhamini pamoja na wadau mbalimbali.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.