Wizara ya Maliasili na Utalii ikiongozwa na Katibu Mkuu wake Dkt. Hassan Abbasi imefanya kikao cha pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Toba Nguvila kujenga mikakati ya pamoja ya kukuza utalii wa Dar es Salaam.
Kikao hicho kimefanyika Desemba 8, 2024 katika ofisi za Bodi ya Utalii (TTB) Dar es salaam na kuhudhriwa pia na Naibu Katibu Mkuu (Utalii), Nkoba Mabula, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Bw. Elihuruma Mabelya na wataalam kutoka Wizarani na Mkoa wa Dar es salaam ambapo kimeweka mikakati mikubwa ya kuifanya Dar es salaam kuwa kitovu cha Utalii wa Mjini (City Tourism).
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.