Tuesday 14th, January 2025
@Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam (City Hall)
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekamilisha maandalizi ya kazi ya kukuza utalii na kuhamasisha watalii wa ndani na nje ya nchi kutembelea Jiji la Dar es Salaam. Kufuatia hatua hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani S. Jaffo (Mb), anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kuanza rasmi kwa kazi hizo kupitia Halmashauri ya Jiji. Uzinduzi huo utafanyika katika Ukumbi wa Jiji (City Hall) tarehe 17 Machi, 2018.
Kazi hizo zitatekelezwa kwa lengo la kuibadili sura ya Jiji kutoka kuwa njia ya kupita watalii na kulifanya Jiji kuwa kituo cha utalii kwa kuongeza muda wa wageni kukaa katika Jiji la Dar es Salaam. Hali halisi ya sasa ni kwamba idadi kubwa ya watalii wafikao nchini hutumia miundombinu na huduma mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam kuwawezesha kwenda kutembelea sehemu nyingine nyingi za nchi na kushindwa kujua kama Dar es Salaam ina sehemu ambazo watalii wanaweza kukaa kabla ya kuendelea na safari zao, na hiyo ni sababu iliyofanya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuamua kuendeleza na kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyoko jijini.
Zaidi ya watu 200 wanatarajiwa kushuhudia kuzinduliwa kwa kazi hizo ikiwa ni hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika sekta ya utalii nchini. Watakaoshiriki katika uzinduzi huo ni viongozi wa Serikali katika ngazi ya Mkoa na Wilaya, Waheshimiwa Madiwani, wadau mbalimbali katika sekta ya utalii na vikundi vya wajasiriamali vinavyoshughulika katika biashara ya utalii katika Jiji la Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.