Na: Shalua Mpanda - Tanga
Timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli imejikuta ikiangukia pua baada ya kuchapwa seti 2-0 na timu ya Dar City katika mchezo wa mpira wa wavu (Volleyball) upande wa wanaume kwenye mchezo mkali uliozikutanisha Timu hizo ndani ya viwanja vya shule ya sekondari Tanga Tech.
Mchezo huo wa mashindano ya Shirikisho la Michezo kwa Serikali za Halmashauri za Mitaa Tanzania(SHIMISEMITA), ukianza kwa tambo kutoka kwa mashabiki wa timu ya Bumbuli ambao mara baada ya mchezo huo kutamatika hawakuamini kilichowakuta.
Dar City ilifanikiwa kuongoza kwa pointi 25-8 katika seti ya kwanza ya mchezo huo kabla ya kuongoza tena seti ya pili iliyoonekana ngumu kwa pointi 25-23.
Kwa ujumla mchezo huo ulikuwa na upinzani mkubwa hasa katika seti ya pili kutokana na uwezo wa wachezaji wa timu ya Bumbuli ambao walionekana kukamia mchezo huo.
Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam maarufu "Dar City" imeweza kuteka hisia za mashabiki wengi katika mashindano haya ambapo imekuwa ikifuatiliwa sana katika michezo yake yote.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.