Dar City yaendelea kutikisa mashindano ya SHIMISEMITA 2025 yanayoendelea Jijini Tanga baada ya kuibuka na ushindi wa kwanza katika mbio kali za 100m relay.
Katika mbio hizo, Jasmine aliongoza kwa kasi ya aina yake kabla ya kumkabidhi kijiti Betila aliyewasha moto zaidi na kuendeleza ushindani. Difna naye hakubaki nyuma, akapiga hatua za kishujaa na kumkabidhi kijiti mchezaji wa mwisho Juliana Lema maarufu kama Mama Mchungaji, ambaye alihitimisha mbio hizo kwa ushindi wa kishindo.
Mashabiki wa Dar City walilipuka kwa shangwe baada ya timu yao kukata utepe wa ushindi na kuonyesha mshikamano wa kipekee katika mchezo huo.
Ushindi huo unaimarisha nafasi ya Dar City kuendelea kuwa tishio na chaguo la kwanza la mashabiki kwenye michezo yote ya SHIMISEMITA 2025
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.